Mwandishi wa Mtandao huu ambaye alisimamia ujenzi wa Nyumba wa Matama toka hatua ya ununuzi wa Kiwanja Mpaka kukamilka kwa nyumba hiyo. kwa kupitia haramnbee iliyoandaliwa na Mtandao huu. Pichani Mwandishi wa Mtandao huu akimkabidhi Pesa Mtama zilizotolewa na Mtandao anayeishi Marekani
Baada ya kununua Kiwanja hicho maeneo ya Kichangani upimaji wa nyumba ukifanyw ana njinia Hayati Mzee Husein ambaye alijitolea kupima na kunjena msingi wa nyumba hiyo bure.
Mwandishi wa Mtandao huu akishiriki kuchimba msingi wa nyumba hiyo
....Nyumba hiyo umefikia hatua ya kupoua
Mjengo umehsapauliwa kwa msaada wa wadau wa Mtandao wa Shekidele
Matama akipanga tafari baada ya hatua ya ujenzi wa msingi kukamilika
Mwandishi wa Mtandao huu akitoa msaada wa unga Sembe kwenye kituo cha watoto yatima cha Mkitnda Kihonda Morogoro.
Mwandishi wa Mtandao huu akitoa msaada wa Pampus kwa mtoto mremavu aliyefichwa na mzazi wake chini ya uvungu kwa zaidi ya miaka 2 kabla ya wananachi wa Dumila kitoa taarifa kwa Mwandishi wa Mtandao huu alifika eneo la tukio na kumfichua mtoto huyo na kumpeleka hospital
MATHAYO.19-16-26
”Na tazama mtu mmoja akamwendea akamwambia Mwalimu,nitende jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?.
Akamwambia kwani kuniuliza habari ya wema ? aliye mwema ni mmoja,lakini ukitaka kuingia katika uzima zishike amri.
Akamwambia zipi? Yesu akasema ni hizi, Usiue,Usizini, Usiibe, Usishuhudie Uongo. Waheshimu baba yako na Mama yako na Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Yule kijana akamwambiya haya yote nimeyashika,nimepungukiwa na nini tena?
. Yesu akamwambia ukitaka kuwa mkamilifu,enenda ukauze ulivyonavyo,uwape masikini nawe utakuwa na hadhina Mbinguni kisha njoo unifuate.
Yule kijana alipolisikia neno lile akaenda zake kwa hudhuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amini nawambieni ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Nawaambia tena ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano ,kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Wanfunzi waliposikia walishangaa Mno,wakisema ni nani basi awezaye kuokoka?. Yesu akawakazia Macho,akawaambia kwa wanadamu hilo haliwezekani bali kwa Mungu yote yawezekana”.Hilo ndilo neon letu la Leo Jumapili ya Agost 7
No comments:
Post a Comment