URAFIKI wa Polisi wa Waandishi wa habari Morogoro unazidi kushika kasi kwa sasa ni vicheko tu kwa Vijana I.G.P Camilius Wambura na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile.
Kufika hapa Pongezi zingi ziwafikie Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya na R.P.C Musilim kwa kurejesha mahusiano mazuri kati ya mihimili hiyo miwili ambayo ni Muhimu sana kwa Jamii ya Wana Morogoro.
Siku za nyuma kabla ya Viongozi hao kuingia madarakani uhusiano kati ya Waandishi wa habari na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro uliregarega baada ya kuondoka kwa R.P.C Thobias Andengenye na RCO wake Ahmed Msangi.
Kwa upande wa MOROPC toka Andengenye alipopata uhamisho, walipita wenyeviti 2 Aziz Msuya na ldda Mushi, wakati Andengenye akiwa RPC Mwenyekiti wa Chama hicho cha Waandishi wa habari alikuwa Boniventure Mtalimbo’Baba Paroko’
Pichani Kigogo wa Polisi Mkoa wa Morogoro Emmanuel Mdhuru akiangua vicheko vya furaha huku akikumbatiana na Waandishi wa habari Hamida Sharrif [Kushoto] na Elizabeth Tanzania [Kulia] anayeshuhudia vicheko hivyo nyuma ni Mwandishi mkongwe mkoa wa Morogoro Alfan Diyu ambaye pia inasemekani ni kocha Mkuu wa bondia Karim Mandonga
Habari na Picha na Dunstan ShekideleMorogoro.
No comments:
Post a Comment