Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, August 4, 2022

MKOA WA MOROGORO UNANYOTA KWA MA- R.P.C.

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabani Tanzania Willibrord Mutafungwa

 Mwandishi wa Mtandao huu kushoto] akimhojiwa Faustan Shilogile ambaye juzi kati aliteuliwa kuwa Mkuu wa Polisi Jamii Tanzania


                                             Na Dunstan Shekidele,Moorogoro
 
. UCHUNGUZI uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu umebaini kwamba Makamanda wengi wa Polisi Mkoa wa Morogoro ‘Ma RPC’ wamepandishiwa vyeo na kuwa Makamishi jambo lililopelekea kuteuliwa kuwa wakuu wa Polisi kwenye vitengo mbali mbali vya Jeshi hilo Tanzania. 
 
Uchunguzi huo umabaini kwamba wa kwanza kupata shavu hilo ni aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Christopher Shekiondo’Msambaa mwenzangu huyu’aliteuliwa kutoka URPC Morogoro na kuwa kamishima na Madawa ya Kuleva Tanzania. 
 
Mwingine ni aliyekuwa RPC Morogoro Rafikia yangu Mkubwa Thobias Andengenye yeye aliteuliwa kuwa Kamishina Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania.baadaye Rais Magufuli alimteua Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma anayehudumu na cheo hicho mpaka sasa.
 
Kama hiyo haitoshi aliyekuwa RPC Morogoro Mama yetu Dorophine Chihallo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Dawati la Jinsia Tanzania, huku aliyekuwa RPC wa Morogoro Wilibrord Mudafungwa aliteuliwa kuwa Mkuu wa kikosi cha Usalaba barabarani Tanzania.
 
Juzikati aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile aliyeuliwa kuwa Mkuu Mpya wa Polisi Jamii Tanzania.
 
Mtandao huu unawapongeza Ma RPC hao kwa kupandishwa vyeo hivyo vikubwa nchini, Mwandishi wa habari hizi anawashauri Vigogo hao wa Polisi nchini kuendelea kutenda haki kwa Jamii ili wazidi kupata baraka za kupandishwa vyeo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...