Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, July 7, 2022

BINGWA WA KUTENGENEZA MABANGO AFUNGUKA ALIVYONUSURIKA KIFO KWENYE AJARI.

Wasaidizi wa Kimti wakiendelea kubandika Bango hilo kwenye Bajaji

 Kimti akiendelea kuweka sawa bango hilo la Kidigital


 

                             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

BINGWA wa Kutengeneza Mabango ya Kisasa ya Digital Mkoani Morogoro Mohamed Faida Branka ‘Maarufu Kimti’amefunguka alivyonusurika kifo kwenye ajari iliyotokea  katikati ya Msitu  Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida wakiwa safarini wakielekea Jijini Mwanza kwenye harusi.

 

 Jana mchana Mwandishi wa Mtandao huu alitinga Makao Makuu ya Ofisi hizo za Kimti Printing Works.

 Warge Format & Digital Printing zilizopo geti namba 1 la Uwanja wa Jamhuri jirani na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro.

 

 

Mwandishi huyo alimshuhudia CEO  wa Kiwanda hicho Kimti akibandika Bango la Kisasa kwenye Bajaj huku akipiga Stori na Mwandishi wa Mtandao huu akimkumbusha walivyonusurika kifo kwenye ajari  mwaka 2009.

 

 Safari hiyo ya kisela sela ilimjumuhisha Mwandishi wa Mtandao huu, Kimti, Samora ambaye anamiliki gereji eneo la Simba Oil, Wema ambaye kwa sasa ni dereva wa kampuni ya mabasi ya Braiton Makundi Maarufu  ‘BM Coach’  pamoja na Cheka Maarufu ‘Don King’ fundi ujenzi na Mwenyekiti wa CUF Kata ya Mji Mpya ambaye kwa sasa ni Marehemu.

 

 

 Kwenye kundi hilo  Madereva wenye leseni walikuwa watatu Samola, Wema na Shekidele hivyo walikatiana kipande vya kuendesha gari hiyo ndogo aina ya Toyota Gx 100.

 

Wema alianza kupiga gia Majira ya saa 5 asubuhi kutoka Morogoro Mpaka Manyoni Mjini, Shekidele anapokea kutoka Manyoni mpaka lgunda Tabora na Samora anamalizia lgunda Mpaka Mwanza.

 

 

 Kwa bahati mbaya tulipofika kwenye msitu wa Manyoni  ghafra tuliona kunakipande cha barabara kinatengenezwa kwa kiwango cha lami,hamadi kwenye kona tukakuta kizuizi kinachotuelekeza kuchepuka kushoto.

 

 Kwa ustadi mkubwa lubani wema alipunguza mwendo na kukwepa kizuizi hicho cha matofali makubwa ya zege na kuparamia msitu ambapo miti hiyo ilipasua taa za mbele, rejeta na sampo.

 

 Kwa Rehema na Neema za Mwenyezi mungu wote nulinusurika ingawa gari iliharibika eneo hilo la Mbele.

 

 Tuliivuta mpaka Manyoni Mjini tukaitengezea usiku huo huo na kulipokucha tukaanza safari ya kuerekea Mwanza, wakati huo ilifika zamu ya Mwandishi wa Mtandao huu kuendesha gari hiyo.

 

 

 Tulipanga kwenda Singiza Mjini kutoa taarifa za ajari hiyo kama sharia inavyoelekeza sambamba na kupewa kibari cha kuendelea na safari tukiwa na hali hiyo ya gari kubondeka, tulivyokaribia Singida Mjini tunapigwa mkono na Trafick  tulivyomkaribia tunabaini ni  Jane Minja Maarufu Jane Bonge aliyekuwa hapa Morogoro.

 

 Niliposimama alivyotuona kangua kicheko na kutuliza tunatoka wapi, tunaenda wapi na ajari hii tumeipata wapi, tukamweleza akatusaidi  kwa kutuongoza sehemu zinazohusika tukakamilisha taratibu zote za kisheria kisha tukapewa kibali cha kuendelea na safari.

 

Wakati Kimtia akiendelea kubandika bango hilo kwenye Bajaj hiyo huku akisaidiwa na wasaidizi wake tuliendelea kupiga stori huku tukimshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yetu kwenye ajari ile.

 

Tulivyomaliza stori hizo tukaingia kwenye stori za utotoni kwani tumesoma shule moja ya kaloleni Primari school iliyopo Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro ambapo moja ya tukio tulilolikumbuka ni adhabu tuliyopewa na Mwalimu Mkamba ya Kuokota Miba aina ya mbiligi  zilizojiotea kwa wingi kwenye eneo la shule akitutaka kujaza bakuri Moja kila mmoja,  kosa letu ni la kutoroka darasani na kwenda kuangalia mazoezi ya timu ya Reli ya Morogoro waliokuwa wakifanya mazoezi asubuhi kwenye uwanja wao uliopo nje ya shule hiyo.

 

 

Vidole vilitoboka toboka kama chujio la Chai baada ya kuchomwa na miba hizo kali wakati tunazichuma, hata hivyo kati yetu hakuna aliyefanikiwa kujaza bakuli la miba hizo japo zilifika robo bakuli.

 

 

 lkumbukwe juzikati  Mh Aziz Abood Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini ambaye pia ni Mmiliki wa kampuni Pendwa ya  Mabasi ya Abood.

 

 

 Alivyonunua mabasi  20 kwa mpigo na kuanzisha ruti za mikoa mbali mbali  Kimti alipewa tenda na tajiri hiyo kutengeza mabango ya Kidigital kama hilo la Bajaj lenye picha za mabasi hayo ambapo kwa sasa mabango hayo yamebandikwa  stend mbali mbali  mikoani.

 

 

Kimti Printing Works bei zake ni nafuu sana ukitaka bango kama hilo la kidigital linalohimilia jua na mvua bei zake ni nafuu peleka Picha yako au tangazo atakutolea kwa bei nafuu sana  wasiliana naye kwa namba 0715 57186.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...