Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KANISA Katoliki Jimbo la Morogoro Juzi Julai 21 limefanya Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 50 ya Upadre wa Askofu Mstaafu wa Jimbo hilo Telesphor Richard Mkude katika kanisa kuu la Mt Patrick Morogoro.
Kabla ya Mwandishi wa habari hizi anayemfahamu vyema Askofu Mkude kueleza tukio kubwa la kuwatetea wanyonge alilolifanya Askofu huyo ambalo mpaka sasa limeacha alama kubwa Jimbo Morogoro, nianze kuelezea histori fupi ya Askofu Mkude.
Mhashamu Askofu Mkude alizaliwa Mwaka 1945 Wilaya ya Mvomero Morogoro, baada ya kuhitimu elimu ya duniani alijiunga na elimu ya dini na kufanikiwa kupata daraja la Upadre Julai 16 -1972 Parokia ya Mgeta Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Januari 18 1988 aliyekuwa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Mtakatifu Yohane Poulo ll alimteua Padre Mkude kuwa Askofu Jimbo Katoliki la Tanga ambapo aliwekwa Wakfu April 26 -1988.
Mwaka 2013 Askofu Mkude alifanya Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu kanisa kuu la Mt Patrick ambapo lbada hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Mh Jakaya Kikwete.
Desemba 30 -2020 Mkuu wa Kanisa Katolini dunia kwa sasa Baba Mtakatifu Francisko alilidhia Ombi la Askofu Mkude kustaafu madaraka yake ya kulitumikia Jimbo Katoliki la Morogoro.
Mwaka 2021 baba Francisko alimteua Padre Vitalis Msimbe kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Morogoro.
ASKOFU MKUDE MTETEZI WA WANYONGE.
Jubilei ya miaka 50 ya Upadre na Uaskofu wa Telesphor Mkude Kwa kinywa kipana Mwandishi wa habari hizi anasema Askofu Mkude ameacha alama ya kuwatetea watu hasa wanyonge.
Binafsi kama nikipata bahati ya kuingia Peponi nisipomuona Askofu Mkude eneo hilo naweza kubeba Ujasili wa kumuliza Mungu mbona simuoni Askofu Mkude kwenye eneo hilo la watakatifu.?
Ushuhuda moja ya utetezi wawanyonge alioufanya Askofu Mkude, nakumbuka takribani miaka 7 iliyopita nikizunguka katika makanisa yote ya Katoliki Jimbo la Morogoro kwa lengo la kupiga Picha za biashara watoto waliohitimu Ekaristi na Kipa lmara nilishuhudia wahitimu hao wakiwa na sale za shule za Msingi wanazosoma.
Tofauti na wale waliopokea Ekaristi hizo miaka ya nyuma ambapo walishindana kwa mavazi ya gharama kubwa kwa watoto wa kiume kuvaa Suti kali huku wale wa kike wakijipodoa na kuvaa mashera kama mabibi harusi.
Baada ya kutolewa kwa agizo hilo la wahitimu wote Kanisa katoliki Jimbo la Morogoro kuvaa sale za shule,waumini waligawanyika makundi kila mmoja akisema lake huku wengine wakipongeza na kundi lingine likipinga.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta Mkuu wa Jimbo hilo Askofu Mkude, alipotakiwa kulitolea ufafanuzi jambo hilo alisema.
“Kwa miaka ya hivi karibuni tumeona kwenye jimbo letu kumekuwa namashindao ya mavazi kwenye Ekaristi na Kipa lmara kati ya wenye nacho na wasio nacho.
Kumekua na muonekana wa wazi wazi kwenye mavazi kati ya watoto wa mataji na watoto wa masikini, hivyo nimeona mashindano hayo ya mavazi wakayafanyie huko ukumbini lakini wakija kanisani kupokea wote wawe sawa kwa maana wavae sale za shule”alisema Askofu huyo.
Kabla ya Jimbo la Morogoro kufikia uamuzi huo kulikuwa na taarifa kwamba kuna mtoto mmoja Muhitimu wa Kipa lmara aliyefiwa na wazazi wake wote wawili[Yatima] ambaye alikuwa akilelewa na bibi yake kijijini alidaiwa kujinyonga hadi kufa kwa hudhuni baada ya kushuhudia wahitimu wenzake wametinga pamba kali Suti na mashera huku yeye akiwa ameva nguo za kawaida tena zenye vilaka vilaka.
lnadaiwa baada ya dogo huyo kutoka kanisa huku akiwa na msongo wa mawazo kwa uchungu, alitafuta kitanzi na kujitundika na moja kwa moja akiwafuata wazazi wake huko wa liko.
Mtandao huu unalipongeza kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro chini ya Askofu Mkude kwa uamuzi huo wa usawa kwa wanafunzi wote kuvaa sale za shule kwa lengo la kuondoa utofauti huo wa walionacho kiuchumi na wasio nacho. Katika mahubiri yake kwenye lbada hiyo ya Misa ya Jubilei juzi Askofu Mkude alitumia sehemu kubwa ya mabubiri yake kuwatetea watu safari hii alijikita kwenye utetezi kwa kuwakemea uharibifu wa mazingira.
No comments:
Post a Comment