Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, July 22, 2022

KUMBUKIZI YA NYOTA WA ZAMANI WA SOKA LA TANZANIA.


Mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union na timu  ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ Kassa Mussa  anayeishi nchini Japan miaka kadhaa iliyopita alijerea nyumbani Tanzania na Moja kwa moja akiwa na wachezaji wenzake nyota wa zamani’Maveterani’ walitinga Makaburi ya Kolla Morogoro na kudhuru katika kaburi la mchezaji mwenzao wa zamani Hayati ldrisa Ngurungu.

 

Baada ya kufika kwenye makaburi hayo Wahenga hao wa Soka la Tanzania walipiga dua kila mmoja kwa lman ya dini yake,baada ya swala na sala hizo Wanasoka hao walipigwa Picha ya pamoja na Mwandishi wa Mtandao huu aliyealikwa kwenye msafara huo.

Pichani Kutoka Kulia ni beki kisisi wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba ya Dar George Masatu’Magele.’ mwenye shati nyeusi ni Hussein Ngurungu kiungo fundi wa zamani wa Pan Afrika ambaye hadi sasa nashikilia rekodi yake ya kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania kwa Miaka 10 rekodi hiyo haijavunjwa na mchezaji yoyote hapa nchini toka miaka ya 80 mpaka sasa.

 

 Kassimu lssa akimshika mkono wa Pole Ngurungu kwa kufiwa na Mdogo wake wa damu, nyuma ya Kassim lssa ni Mohamed Mtono beki wa zamani wa Reli ya Morogoro.

 

 Na kulia kwa Kassim lssa ni Ally Jangaru’Mwananguuuu’ ambaye ni mchezaji wa zamani wa Reli ya Morogoro.na Pan Afrika pia msimu uliopita alikuwa kocha Msaidizi wa Kagera Sugar  wa mwisho ni beki wa zamani wa Reli Hamis Malifedha’Mnyamwezi’.

 

Hayati ldrisa enzi za uhai wake aliwahi kuzitumikia timu za Reli ya Morogoro. Pan Afrika, Coastal Union na timu ya taifa ya Tanzania’Taifa Stars.

 

        KIFO CHA NGURUNGU.

 

Hayati ldrisa Ngurungu akiwa mmoja wa waombolezaji waliotoka Morogoro mjini kwenda kuzika Matombo  Wilaya ya Morogoro Vijini, wakati wanareja Morogoro Mjini gari hilo lililobeba waombolezaji lilipata ajari eneo la Mkuyuni ambapo ldrisa pekee ndiye aliyefariki dunia papo hapo huku wengine wakijeruhiwa.

 

“ Fundi wa Mpira ldrisa Ngurungu Mwana wa Pakaya umezimika kama Mshumaa nenda kamanda Mwendo umeumaliza tutaonana badae lnnalillah wainaillah rajiun”

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...