. Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
HII NI AIBU .
TIMU 18 za Wilaya ya Morogoro zimeangumkia pua kwenye michuano ya Vijana wa Umri chini ya Miaka 20 na kuziacha timu mbili zilizokaribishwa kwenye michuano hiyo kutoka Wilaya nyingine kucheza fainali kesho kwenye michuano
hiyo iliyoandaliwa na Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’.
lfahamike Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’ kupitia kwa Rais wa shirikisho hilo Walles Karia aliviangiza vyama vyote vya Soka Wilaya ya Mikoa kuanda michuano ya Vijana pamoja na Soka la Wanawake kwenye maeneo yao. Hivyo chama cha Soka Wilaya ya Morogoro liamua kutii agizo hilo kwa kuanzisha michuano hiyo iliyoshirikisha timu 18 kutoka kwenye Wilaya hiyo.
Timu hizo ni SUA Academy,Moro Youth, Mega Sports Kihonda United, Moro Kids. Black Viba, Save Talents, na Chamwino Youth.
Nyingine ni Jamhuri Boys, New Kings, Tanzanite, Burkina Faso. Motasoa. Kaizer Chief. Moro Boys Sports, New Ngerengere, Mkundi Youth, Mafisa United, na Misongeni Fc.
Baada ya tangazo la kuanzishwa michuano hiyo kutolewa kwenye nyombo vya habari timu 3 kutoka Wilaya na mikoa Mingine zilituma maombi ya kushiriki michuano hiyo, kufuatia Wilaya zao kutoandaa mashindano hayo.
Timu hizo zilizoomba na kukubariwa ni Kilombero Soccer Net Kutoka lfakara Wilaya ya Kilombero, Kikosi cha Pili cha timu ya Ligi kuu Maafande wa Ruvu Shooting ‘Under Twenty’ Kutoka Mlandizi Mkoa wa Pwani na Pwani Sports Foundation pia Pwani.
Michuano hiyo iliyopigwa uwanja wa Saba saba kwa takribani miezi 2 inafika tamani Kesho kwa timu za Ruvu Shooting na Kilombeso kucheza fainali huku timu wenyeji 18 zikiketi jukwaani kushuhudia fainali hiyo ambayo mshindi wa kwanza anatarajiw akupewa zawadi ya seti mbili za Jezi na kikombe huku mshindi wa Pili akitarajiwa kupewa seti moja ya Jezi.
Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba kuferi kwa timu hizo 18 za Wilaya ya Morogoro ni tamaa za mshika mawili hukosa yote.
Uchunguzi huo umebaini kwamba baadhi ya taasisi za soka zenye upinzani mkali wilaya ya Morogoro zimeamua kujigawa nakuingiza timu 3 kwenye michuano hiyo huku timu nyingine zikijigawa na kushiriki michuano ya Ndondo Cup inayoendelea jijini Dar es salaam.
Taasisi ya Moro Kids badala ya kutengeneza timu moja yenye ushindani yenyewe imejigawa na kuingiza timu 3 ambazo ni Moro Youth, Moro Kids na Jamhuri Ball Boys.
Huku taasisi ya Tanzanite nayo ikijigawa na kuingiza timu mbili za Motasoa na Tanzanite.
Kwa pande wa Black Viba iliyoepewa nbafasi kubwa ya kutwaa taji hilo ilijikuta ikitolewa kwenye robo fainali na Chamwino Youth kufutia siku hiyo hiyo ya mchezo huo wachezaji wao nyota zaidi 9 siku hiyo walikwenda Dar na timu ya Moto Town kwenye michuanoi ya Ndondo Cup.
Leo kunagemu ya kumsaka mshindi wa tatu kati ya Burkina faso na Motasoma na kesho Mwandishi wa Mtandao huu atakuwepo kwenye mchezo wa leo na ule wa fainali kukusanya matukio hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
Picha juu ni wanafainali ‘Wajeda’ JKT Ruvu Shooting kutoka Mabatini Mlandizi Pwani.
No comments:
Post a Comment