lkumbukwe Messi alikuwa kuichezea Geita Gold kwa mafanikio makubwa wakati huo ikiwa daraja la kwanza kabla ya mchezaji huyo kujiondoa kwenye kwenye timu hiyo na kutimkia timu za Zanzibar. Baada ya gemu hiyo kutamatika Mwandishi wa habari hizi alimfuta mchezaji huyo na kumuliza kwa sasa anakipiga timu gani ambapo alijibu.
" Broo Shekidele kwa sasa niko kwenye mazunguzo ya mwisho na Uongozi wa Mtibwa Sugar hivyo mambo yakienda vizuri msimu ujao nitakuwa Mtibwa Sugar"
Messi wa Chamino akielekea kwenye Kibendera kutetema baada ya kufunga bao
Kipa wa Chadongo Fc Hussein Dior ambaye pia ni kipa wa Simba B akiluka bila mafanikio kujaribu kuzuia shuti kali la mshambuliaji wa Wakushi aliyeipatia timu yake bao la kufutia machozi.
Winga wa Wakushi Fc akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Chadongo
Utamu wa Picha hii ni umakini wa refa kwenye tukio hilo linaloendela ndani ya eneo la 18, mabeki wakijichanganya tu amefunika tuta
Mwamuzi James Andrew aliyemudu nyema mchezo huo akiamuru upigwe mpira wa adhabu ndogo kuelekea lango la Chadongo ambapo baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakionekana kupingana na maamuzi ya refa huyo wa daraja la Kwanza
Kipa wa Chadongo Fc Hussein Dior anayekipiga Simba B ambaye ni Mkazi wa Dumila Morogoro
Kiungo fundi wa Chadongo Fc, Twaribu Chacharo anayekipiga timu ya daraja la kwanza Pitayosi ya Tabora inayoongozwa na rafiki yangu Yusuf Kitumbo.
Kipa wa Chadogo Hussein akinyaka mpira kama nyamani
Mshambuliaji wa Wakushi Fc Mohamed Kijiko, huyu aliwahi kukipiga Simba na Coastal Union ya Tanga
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
UTAMU
umerejea ile mchuano Pendwa ya The Gunners Ndondo Cup imezinguliwa juzi Uwanja wa Saba saba Morogoro kwa mchezo wa Mtani
Jembe kati ya Mabingwa watetezi, Wakushi Fc kutoka Manzese Morogoro na Chadongo
Fc.
.
Katika mchezo huo uliojaa mastaa kibao kutoka timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na daraja la Pili ulitamatika kwa Chadongo kuibuka na ushindi wa bao 2-1.na kujinyakulia zawadi la pesa laki tano taslimu.
Gemu hiyo iliyao kuwa na upinza mkali kwa Muda wote wa dakika 90 ulihudhuriwa na beki kisiki wa Yanga na timu ya Tifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mluguru Kibwana Shomari aliyekuwa jukwaani akishuhudia miamba hiyo ikipepetana.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kibwana alisema mara baada ya kuitumikia timu ya taifa kwenye michuano ya Kimataifa, amereja nyumbani Morogoro kwa mapunziko mafupi kabla ya kujiunga na kambi ya timu yake ya Yanga.
Alipoulizwa kama atauwahi mchezo wa Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga utakaopigwa leo saa 2 Usiku Uwanja wa kumbukumbu ya Mkapa uliopo Temeke Dar ambapo kama yanga ikifanikiwa kushinda itanyakua Ubingwa wao ligi hiyo uliokuwa mikononi mwa Simba kwa misimu 3 mfurulizo.
Hataku sehemu ya mchezo huo kufuatia kuwa na kadi tatu za njano zinazomzuia kucheza mchezo huo, ukitaka kuona picha zaidi za matukio ya mchezo huo na Picha za mastaa hao wa ligi kuu ingia www.shekideletz.blogspot.com.
Kivutia kikubw akwenye Pichani hii ni umakini wa Mwamuzi wa mchezo huo James Andrew mchezki alivyokuwa makini kuangalia wanaume wanavyopambana ndani ya eneo la 18.
No comments:
Post a Comment