Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 27, 2022

WAKUSHI FC WATINGA FAINALI MICHUANOI YA PLANET NDONDO CUP.

                                    Kikosi cha wakushi Fc
                                 Kikosi cha Black Viba


Mashabiki lia lia wa Viba Mapacha wawili wakipozi mbele ya kamera za mtandao huu baada ya kuingia uwanjani






Mshambuliaji wa Wakushi Fc Mwashinya Emmanuel Jezi no 7 mgongoni akipachika bao la pili kw atimu yake na kumwacha kipa wa Viba Gumbo Mfaule akiruka bila mafanikio

Mashabiki wakimpongeza  Emmanuel baada ya kufunga bao hilo
Kipa wa Wakuhsi Fc Omary Pande akiruka juu kuondosha mpira uliokuwa ukielekea wavuni. katika mchezo huo kipa huyo alifuta mabao mengi ya wazi .likiwemo bao hili.


Kipa wa Viba Mfaume Gumbo ambaye pia ni kipa namba moja wa Gwambi Fc ya Misungwi Mwanza akiruka juu kunyaka mpira. lkumbukwe kabla ya kujiunga na Gwambina Gumbo alikuwa kipa namba moja wa Mawenzi Market ya Mkoani Moorogoro.

Kipa wa Viba Gumbo Mfaume mpira umempita ikielekea langoni.
...Beki kisiki Nassoro Ndunga'Choro' aliibuka na kuondoka mpira huo kabla haujaingia gorini. Choro ni beki wa zamani wa Mawenzi Market iliyoshiriki,ligi daraja la kwanza.
Mwamuzi wa Ally Mnyumbe ambaye kwa sasani anachezesha ligi kuu ta Tanzania Bara akimwalika daktari kuingia uwanjani kumpa huduma beki wa Wakushi Fc Yunus  Dadi ambaye pia ni beki kisiki wa timu ya Dar City ya jijini Dar.

Yunus Mkazi wa Mifufini Mafika mkoano hapa aliumia baada ya kubabuliw ana mpira kifuani eneo ambalo moyo unadunda




 Kiongozi wa timu ya Wakuhsi Fc Chacha Marwa[kulia] mwenye flana yenye nchata la bendera ya Marekani naye alishiriki kuingia uwanjani kutoa msaada ya yunus


 

 

                                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

TIMU ya Wakushi Fc ‘Chuma cha Mjerumani’ juzi ljumaa wametinga fainali ya Michuani ya Planet ndondo Cup baada ya kuwanyuka wapinzani wao wakubwa Black Viba kwa bao 2-0.

 

Licha ya upinzani mkali walioupata kwa Muda wote wa dakika 90 toka kwa majirani zao hao lakini Wakushi Fc walitumia mbinu za ziada na kufanikiwa kupta bao la kwanza dakika 20 kupitia kwa Stam Odasi aliyemchambua kipa wa Viba Gumbo Mfaume na kupachika mpira wavuni.

 

 

Baada ya kufungwa bao hilo beki ya Viba iliyokuwa chini ya Yunus Dadi anayekipiga  Dar City ya Jijini Dar na Kipa wao Gumbo Mfaume anayeidakia Gwambina Fc ya Misungwi Mwanza iliyumba yumba kama dera na kujikuta ikipachikwa bao la Pili kupitia kwa mshambuliaji wa Wakushi Fc Mwashinya Emmanuel.

 

Kufuati ushindi huo Wakushi Fc wametinga fainali ya michuano hiyo ambapo ljumaa ijayo watakipiga na Chadongo Fc kwenye mchezo huo wa fainali na bingwa atakabidhi kitita cha shilingi milio 3 taslim.

                        PONGEZI KWA WAANDAJI.  

Michuano hiyo ya Planet Ndondo Cup imeandaliwa na kituo Pendwa cha Planet Redio cha Mkoani hapa.

 

Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha timu 4,kati ya Chadongo Fc na Black People Mtandao huu uliripoti  kusoro iliyojitokeza kwenye mchezo huo.

 

 Kasoro hiyo ni karatazi za majina ya wachezaji wa timu zote mbili kuandikwa jina moja moja la wachezaji badara ya majira kamili 2.

 

 

Kwenye mchezo wa juzi ljumaa waandaji wa michuano hiyo kupitia kwa Mc Salum Mapande ambaye pia ni Mchambuzi Maarufu wa kipindi cha Michezo wa Redio hiyo alikamata Mic na kuwatangazia Viongozi wa timu zote mbili kuhakikisha Karatazi za maiina ya wachezaji wao yanaorodhesha kikamilifu.

 

Kwa msisitizo Mapande alililudia tangazo hiyo zaidi ya mara mbili ambapo Viongozi wa timu hizo kweli walitii agizo hilo na kuwasilisha karatazi hizo za majina zikiwa na majina kama kama zinavyoonekana Pichana.

 

Kama kawaida katika mchezo huo  Mtandao huu umekusanya matukio kibao likiwemo tukio la Mashabiki wa Black Vina na Wakushi Fc kutwangana Makonde wakigombea Mpira hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu  kushuhudia washabiki hao wakitandikana makonde.  

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...