NIMELIPATA MATHAYO 5. 43-48
“Nimesikia kwamba imenenwa, umpende jirani yako na umchukie dui yako.
Lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu,waombeeni wanaowaudhi.
lli mpate kuwa wana wa baba yenu aliyembinguni,maana yeye huwangazia jua lake waovu na wema,huwanyeshea mvua wenye haki na wasi haki.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani?.
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu,mnatenda tendo gani la ziada?.
Hata watu wa mataifa je, Nao hawafanyi kama hayo?
Basi ninyi mtakuwa wakamilifu,kama baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”
UFAFANUZI WA SOMO HILO.
Moja ya tunda la roho ni Upendo na Upendo uliozungumziwa kwenye neno hili la Mungu ni ule Upendo usio hesabu mabaya.
Upendo wa kweli ni Upendo wa Matendo sio ule wa kutamka mdomoni, na kipimo cha Upendo wa kweli ni kwenye shida.
Mfano Umemkosea rafiki yako, ndugu yako,Mpenzi wako au mke wako kipima chake cha Upenzo ukipima kwenye eneo hilo.
Neno la Mungu hapo juu limefafanua vizuri hakuna faina kubwa kumpenda anaye kupenda faina kubwa utaipate pale utakapompenda aliyekukosea ndio utafananishwa na Mungu.
Neno hapo juu limetoa mfano wa Mungu anavyo toa haki kwa waovu na wenye haki Mfano mtu analima zao la haki Mahindi na mwingine analima zo la haramu Bangi lakini Mungu huyo huyo anawapa mvua na jua wakulima wote hao bila ubaguzi.
Tusiishi kwa kuwawekeka visasi waliotukosea tutafute amani ya moyo kwa waliotukosea huo ndio Upendo wa kweli anaouhitaji Mungu.
lfahamike kumpenda anayekupenda sio dhambi ila kumpenda aliyekuudhi au aliyekukosea ni jambo jema zaidi na huo ndio Upendo wa kweli na wa matendo.
Kinyume cha tunda la Upendo ni Chuki kwa maana ya kumchukia aliyekuudhi au kukokosea.
Neno hilo la limehitimishwa kwa kutuelekeza kwamba tukifanya hayo tutakuwa wakamilifu kama baba yengu wa mbingu ‘Mungu’alivyo mkamilifu.
Kwa leo mtumishi wako Dunstan Shekidele anaishia hapa hivyo ikimpendeza Mungu tukutane Jumapili ijayo kwa somo lingine Mungu awabariki wote mliosoma neno hili.
Mwenye Masikio na asikie asiye na Masikio […….]
CAPTION.
Pichani nikifanya mahojiano na aliyekuwa Askofu Msaidizi wa KKKT Dayosisi ya Morogoro Mch George Pindua ndani ya ofisi za Dayosisi hiyo zilizopo Usharika wa Mji Mpya.
No comments:
Post a Comment