Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, June 29, 2022

WAKATI LIGI KUU IKIFIKA TAMATI LEO. MORO KIDS WAIBUKA USAJIRI KIPA WA YANGA.



 


 

                               Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 

 WAKATI msimu wa ligi kuu Tanzania Bara, ukifika tamati leo, Uongozi wa Taasisi Maarufu nchini ya kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji ya Moro Kids  ya Mkoani hapa,wameibuka na kudai Pesa yao  ya Usajiri wa Kipa mpya wa Yanga Abuutwarib Msheri.

 

 

Majuzi Mwandishi wa Mtandao  huu akiwa kwenye mishe mishe zake za kusaka matukio alipigiwa simu na Mratibu Mkuu wa Taasisi hiyo Rajab Kindagule akimwalika kufika kwenye taasisi hiyo.

 

”Shekidele tunajua Mtandao wako unawasomaji wengi, njoo hapa Mazoezini kwetu Uwanja wa Shujaa tukupe habari inayomhusu Kipa wa Yanga Msheri”

 

 Fasta Mwandishi wa Mtandao huu alitinga eneo la tukio na Moja kwa moja Mratibu huyo alifunguka haya.

 

”Kama taasisi tumekuita kutoa lalamiko letu ligi kuu inafika tamati jumatano Mpaka leo Mtibwa hawajatulipa pesa yetu waliyomuuza Kipa Msheri kwenda Yanga kama tulivyokubaliana kwenye mikataba yetu”.alisema Kindagule na kuongeza.

 

 Haya tunayaona siku hizi lakini enzi la Uongozi wa Jamal tulikuwa tunalipwa haki yetu kwa wakati wanapomuuza mchezji wetu wanatupa haki yetu, nakumbuka mzozo ulianzia kwa Dickson Job tulihangaika sana kulipwa pesa yetu mpata tulivyowapeleka Mtibwa Takukuru ndio wametulipa Malipo ya Job.

 

 Kama taasisi tumeona lalamiko letu tulipeleke kwenu Waandishi wa habari mtusaidie kupaza sauti”amemalizia kusema Mratibu huyo ambaye ni Mwamuzi Mstaafu wa ligi Kuu Tanzania Bara.

 

Alipouliza Malipo hayo wanayoda ni kiasi gani, alisema makubaliyao yao kwenye mkatani wa Kipa huyo ni kwamba atakapouzwa popote Moro Kids watalipwa asilimia 25 ya pesa za mauzo.

 

 Alipoulizwa swali la pili kwa sasa taasisi hiyo ya Moro kids inawachezaji wangapi waliobaki kwenye kikosi hicho cha Mtibwa kwa sasa. alijibu

 

 “Tunawachezaji kama watano hivi kwenye kikosi cha Mtibwa na kwenye kikosi chao cha pili asilimia 80 ya wachezaji wote wa timu B ya Mtibwa wanatoka kwenye taasisi yetu.

 

Baada ya kusikia malalamiko hayo jana Mwandishi wa habari hizi aliwatafuta Viongozi wa Mtibwa kwa njia ya simu kwa lengo la kusikia kauli yao juu la lalamiko hilo zidi yao.

 

 Aliposomewa malalamiko hayo na kutakiwa kuyatolea majibu Kiongozi wa Mtibwa aliyejitambulisha kwa jina Moja la Abubakar alisema.

 

” Ni kweli Moro kids wanatudai hiyo pesa ila utaratibu walioutumia wa kuja kwenu Waandishi wa habari binafsi sikuupenda na juzi tu nimeongea na Kindagule nikimuomba waendelee kutuvumilia”alisema Kiongozi huyo.

 

 Alipoulizwa kwa nini wasilipe deni hilo ili hali wameshamuuza mchezaji huyo? Kiongozi huyo alijibu.

 

”Niwe mkweli  Yanga hawajatulipa pesa yetu ndio maana nikamwambia Kindagule aendelee kutuvumilia tulipipwa na Yanga na sisi tutawalipa pesa yao”alisema Kiongozi huyo.

 

  Alipoulizwa tena kwa nini wamekubali kumtoa Kipa wao Muhimu bila kulipwa pesa ili hali wakijua mchezaji huyo sio mali yao peke yao kuna taasisi iliyoibua na kukuza kipaji chak.?

 

 Kiongozi huyo hakujibu swali hilo na badala yake alikata simu.

 

 

Siku za nyuma sakata hilo liliibuka kweny vyombo vya habari ambapo Uongozi wa yanga urikaririwa ukidai kwamba umesharipa malipo ya Kipa huyo na hawadai chochote.

 

Baadhi ya wachezaji wa Moro Kids waliotimkia timu mbali mbali zikiwemo Simba na Yanga waliouzwa na Mtibwa Sugar ni Pamoja na Shomari Kapombe, na Mzamiru Yasini Simba.

 

 Dickson Job, Shomari Kibwana na Kipa Abuutwarib msheri[Yanga] Shiza Kichuya, [Namungo].Hassan Kessy[KMC] Juma Abdul Singida Big Stars na Hamad Waziri’Kuku [Mbeya City]

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...