Mmiliki wa nyumba hiyo Kada wa CCM Nasma Ndehere akitoa maelezo kwa Afande wa kikosi cha Zima Moto
Afande wa kikosi cha Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro akiendelea kuzima Moto kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo
Ponge za kipee zimfikie Afande huyu aliyefika mapema eneo la tukio la kulinda mali zilizokuwa zikiokolewa kutoka kwenye nyumba hiyo.
....Afande huyo akimfariji Mmili wa nyumba hiyo Bi Nasma Ndehere
..Mmoja wa wapangaji aliyedaiwa kujiandaa kuhama kwenye nyumba hiyo akiangua kilio baada ya baadhi ya vitu vyake kuteketea kwa Moto.
Katibu Mwenyezi wa CCM Kata ya Mji Mpya Seleman Kasanga shati jekundu] akimsaidia mpangaji huyo kuokoa vitu kutoka kwenye janga hilo la Moto
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
INAUMA SANA.
Nyumba ya Nasma Hamisi Ndehere ambaye ni Kada Maarufu wa Chama Cha Mapinduzi’CCM’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, imeteketea kwa Moto huku mgonjwa aliyekuwa amelala ndani akinusurika baada ya kuokolewa na majirani.
Tukio hilo la kuhudhunisha limetokea jana mchana kwenye nyumba hiyo ya familia ya Ndehere iliyopo Mtaa wa Makaburi B kata ya Mji Mpya.
Mwandishi wa Mtandao huu aliyekwenda kumsalimia Bi.mkubwa wake anayeishi kwenye Mtaa huo. alishuhudia watu wakikimbia huku wakipiga kelele za nyumba inaunga.
Mwandishi wa habari hizi naye alikurupuka na kutinga eneo la tukio na kushuhudia moto huo ukianza kushika kasi, Moja kwa moja Mwandishi huyo alipiga simu Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji kupitia namba yao ya bure’Emergency Number’ ya 114.
Ndani ya dakika chache maafande hao wa Zima Moto walitinga eneo la tukio na kuzima moto huo ambao tayari ulikuwa umeshateketeza vyumba 2.
Akizungumza na Mtandao huu kada huyo wa CCM ambaye pia ni Mshereheshaji ’Mc’ Maarufu Mkoani Morogoro alisema.
”Nilikuwa kwenye shughuri zangu Mtaani nimepigiwa simu nikijulishwa nyumba yetu inaungua moja kwa moja nilimuwaza mgonjwa wangu aliyekuwa amelala ndani na pesa za watu za mchezao Laki 2 zilizozihifadhi chumbani.
“Nashukuru nimefika hapa nimekuta majirani zangu wamemuokoa Mgonjwa na kwa vile moto ulikuwa haujafika chumbani kwangu nilimtuma kijana kazitoa pesa hizo”alisema Mc Nasma ambaye pia ni Mke halali wa Hamis Ndehere.
Katika hatua nyingine Mc Ndehere alimuelekeza kwa hema Mpangaji wake aliyekuwa akifoka baada ya Moto huo kuunguza baadhi ya vitu vyake.
Mpangaji huyo Pichani anayeangua Kilio, kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana eneo la tukio alikuwa akijianda kuhama kwenye nyumba hiyo alikuwa akisubiri Muda ufike kama utamaduni wetu ulivyo wa kuhama majira ya Usiku.
Kwa bahati mbaya wakati akisubiri hilo na yeye akiwa kwenye ,majukumu yake Mtaani alipigiwa simu akijulishwa tukio hilo la Moto.
Aliwasili eneo la tukio kwa usafiri wa boda boda na moja kwa moja alikimbilia chumbani wake kuokoa baadhi ya vitu huku akiangua kilio akitaka kulipwa vitu vyake vilivyoungua.
Mama mwenye nyumba Mc Nasma baada ya kumsikia mpangaji wake huyo akifoka alimfuata na kumueleza kwa hekima.
“Nimekusikia ukilia huku ukilalamika ukitaka kulipwa vitu vyako,hakuna mtu aliyependa nyumba kungua hii ni ajari kama ajari nyingine hivyo unavyolalamika kungua kwa vitu vyako, wakati na mimi ninauchungu nyumba yangu kungua”.
Maneno hayo ya hekima yalimgusa mpangaji huyo na Mwandishi wa Mtandao huu alimsikia mpangaji huyo akisema neno moja tu.
“ sawa mama lakini vitu hivi vichache nilivyookoa haviludi tena kwenye nyumbani hii naita gari naondoka zangu.”
Mwenye nyumba huyo hakumjibu chochote mpangaji wake huyo na badala yake aliondoka eneo hilo na kwenda kutoa maelezo ya tukio hilo kwa maafisa wa Kikosi cha Zima Moto. Mtandao huu uliwashuhudia Vigogo kibao wa CCM Kata ya Mji Mpta wakishiriki kumsaidia Kiongozi mwenzao kwenye janga hilo.
Baadhi ya Kigogo hao wa CCM walioshuhudia na Mwandishi wa habari hizi ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM kata ya Mji Mpya Said Kondo, Katibu Mwenezi Kata Seleman Kasanga, na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Simu C kata ya Mji Mpya kwa leseni ya CCM Said Mkwinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro.
.
Hadi tuna kwenda mitamboni chanzo cha Moto huo hakijajulikana na hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa zaidi ya baadhi ya mali kuteketezwa na Moto huo.
No comments:
Post a Comment