Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, June 24, 2022

BAND YA WALUGURU OG KUNOGESHA UBINGWA WA YANGA LEO JIJINI MBEYA





 

HII IMEKAA VIZURI.
 
                                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
Band Maafuru kwa sasa Tanzania Waluguru Original ya Mkoani hapa, Jana wametinga Jijini Mbeya kwa lengo la kunogesha Ubingwa wa Yanga watakaokabidhiwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine, baada ya kutamatika kwa mchezo wa ligi kuu dhizi ya wenyeji wao Mbeya City utakaopigwa majira ya saa 10 jion. 
 
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi jana muda mfupi kabla ya kuondoka Kiongozi wa band hiyo Deogratius Arophonce Maarufu Killer Boy amesema leo Jumamosi watauwasha moto mkali kwenye ukumbi wa City Pub ulipo Mbeya Mjini kuanzia saa 1 usiku mpaka Usiku Mnene.
“ Shekidele tumekodi hii basi nafasi lpo kama hauko bize kikazi twende Mbeya”, alisema Killer boy na kuendelea kufunguka juu ya safari hiyo ya Kijanja.
 
"Muda huu tunaelekea Jijini Mbeya Kesho Jumamosi tukipiga shoo ukumbi wa City Pub jumapili tutapiga tena kwenye ukumbi huo huo na jumatatu kutaelekea Tunduma nako tutakiwasha kabla ya kureja nyumbani Morogoro,
 
Alhamisi ratiba yetu itaendelea kama kawada kwenye kumbi za hapa nyumbani”alisema Mmiliki wa band hiyo Killer Boy Mluguru wa Matombo Mkuyuni.
 
Haya mashabiki wa Yanga burudani hiyo baada ya kukabidhiwa kombe lenu leo majira ya saa 12 jioni Mida ya saa 1 sogeeni hapo City Pub mpate burudani kali kutoka kwa Vijana ya Mji kasoro Bahari’Waluguru Og Band.’
 
Tutokana na ubora wa Band hiyo kila mara inapata mwaliko kwenye majiji mbali mbali ya Tanzania ambapo hivi karibuni alialikwa Jijini Mwanza. Walipotoka huko wakapata mwaliko Jijini Arusha na juzi kati walipata Mwaliko Jijini Dar es Salaam na Jana wamepata Mwaliko Jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...