Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, June 11, 2022

PAPARAZI APANGUA HOJA YA KIGOGO WA POLISI.




   RCO akichangia Madai hiyo huku akitoa duku duku lake


                              Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 
Mwandishi wa habari ‘Paparazi’ wa Mtandao huu Juzi June 8 amepangua shutuma za Kigogo wa Polisi Mkoa wa Morogoro juu ya habari zinazoandikwa na Waandishi wa habari zinazolihusu Jeshi hilo la Polisi.
 
Hayo yaliibuka kwenye Mdahalo uliondaliwa na Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ uliokuwa na agenda moja tu ‘Juu ya Ulinzi na Usalama wa Mwandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro’
 
.Mdahalo huo ambao Mgeni rasm alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, aliyewakirishwa na Kaimu RAS Dr Rosalia Rwegasira, ulihudhuriwa na Makamanda wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Morogoro pamoja na wenyeji Waandishi wa habari wa Mkoa huo. 
 
Baada ya mdahalo kufunguliwa agenda hiyo ilianza kudadavuliwa huku kila Upande ukitoa duku duku lake kabla ya kuchangia agenda hiyo. 
 
Ilipofika zamu ya Jeshi la Polisi kuchangia agenda hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishina Msaidizi wa Polisi’ Ralph Meela ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro’R.C.O’ alianza kwa kutoa duku duku lake alisema.
 
”Kuna baadhi ya waandishi wa habari wanaandika habari zinazotisha wageni kuja kwenye mkoa wetu mfano ukiandika habari inayosema ujambazi umekidhiri Morogoro, mtu wa Mkoa mwingine akisoma habari hiyo ataogopa kuja Morogoro”alisema R.C.O Meela.
 
Baadaye Mwandishi wa Mtandao huu alipewa nafasi ya kuchangia agenda hiyo ambapo kabla ya kuchangia alimjibu Kamanda Meela
”Kabla sijachangia nimjibu R.C.O Meela kwamba neon kukidhiri ni mwendelezo wa tukio hivyo kama tukio linajiludia zaidi ya mara 3 sio dhambi Mwandishi kuandika hivyo.
 
“Mfano Kilosa Polisi walituhumiwa kuua mtuhumiwa, juzikati tumesikia tena Polisi wametumiwa kuuwa mtuhumiwa maeneo ya Mvua, tukisikia tena Polisi wanatumuhiwa kuua mtu Mvomero Mwandishi taandika matukio ya Polisi Morogoro kudaiwa kuuwa watuhumiwa yamekidhiri”alisema Shekidele.
 
Baada ya majibu hayo Mwandishi wa Mtandao huu naye aliamua kutoa duku duku lake kwa Jeshi la Polisi akieleza alivyovamiwa na Polisi kwenye matukio mbali mbali akizuiwa kufanya kazi yake.
 
Vuluguru hizo walizofanya baadhi ya Polisi wachache zilisababisha kukatika kwa Rozari aliyokuwa amevaa shingoni Mwandishi huyo, huku tukio lingine Polisi waking’ang’ania kamera ya Mwandishi wa Mtandao huu kiasi cha Kupoteza Berti la kamera hiyo.
 
Tukio hilo lilimkera aliyekuwa RPC wa Morogoro Urlch Matei ambaye kwa sasa ni RPC wa Mkoa wa Mbeya aliamuru Polisi huyo kulipa Betri hilo.
 
Habari hiyo itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
 
                          CAPTION
RCO Meela akichangia kwenye Mdahalo huo.
Mwandishi wa Mtandao huu wa kwanza kushoto waliochuchumaa aliyevaa jezi ya Bluu ya timu ya Taifa ya Tanzania akiwa katika Picha ya Group na wadau wote wa mdahalo huo nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...