Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 12, 2022

MWANDISHI ATOA DUKU DUKU LAKE KWENYE MDAHALO.

 

Na Mwandishi Wetu Morogoro.
 
LEO tunamalizia simulizi yetu ya Mdahalo wa Wandishi wa habari na Wadau wa habari kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Morogoro.
 
Kwenye Mdahalo huo uliofanyika June 8 ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kila upande ulitoa duku duku lake kabla ya kuchangia Mada husika.
 
Miongoni mwa Waandishi waliotema nyongo kwa makamanda hao wa Ulinzi na Usalama ni Dunstan Shekidele,ambaye alielezea alivyonyanyaswa na Polisi kwenye matukio mbali mbali. 
 
MSIKIE MWANDISHI HUYO AKITEMA NYONGO.
 
”Mimi ni Mwandishi wa habari za Kijamii na Uchunguzi, hivyo nimekuwa karibu zaidi na Jamii ambapo linapotokea tukio Mtaani mara nyingi nimekuwa wa kwanza kupigiwa simu na Wadau wangu hao.
 
“Hivyo nikifika kwenye tukio nikiona Polisi hawapo huwa na mpigia simu RPC au OCD kumpa taarifa ambapo fasta hutuma Vijana wake eneo la tukio.
 
Chaajabu bila kujua kama mimi ndio niliyetoa taarifa kwa mabosi wao baadhi ya Polisi wenye vyeo vya chini wanapofika eneo la tukio wanaanza kunifanyia vulugu wakizuia nisifanye kazi yake ya kupiga Picha.
 
Kama agenda yetu inavyosema ‘Ulinzi na Usalama wa Mwandishi wa habari Mkoani Morogoro’Ninaushahidi wa matukio Mawili niliyofanyiwa vulugu na Polisi nikiwa kazini.
Tukio la Kwanza nakumbuka ni takribani miaka 5 iliyopita kuna mauaji yalitokea eneo la Mazimbu Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 SUA Campas ya Mazimbu alidaiwa kumuua Mpenzi wake wakiwa gest huku chanzo cha mauaji hayo inadaiwa dent huyo kutoka Mkoa wa Mara alimshutumu mpenzi wake huyo kumwambukiza maradhi.
 
Wananchi walinipa taarifa za tukio hilo, nilipofika sikuwakuta Polisi nikaamua kuwajulisha.
Fasta Difenda lilifika likiwa na kiongozi Afande Bitrice Lyamuya mwenye cheo cha nyota 2.
Wakati Polisi wakitoa Mwili wa marehemu huyo aliyekuwa muhudumu wa Gest hiyo na stecha huku wakiwa wameufunika na shuka nilifanya kazi yangu ya kupiga Picha kwa lengo la kuhabarisha umma wa watanzania. 
 
Chaajabu mmoja wa Polisi aliyeshika bunduki alinivamia kwa nyuma akanikaba shingo na kukata Rozari nikamsukuma nakufanikiwa kutoa kabari hiyo, huku kundi la wananchi waliofulika eneo la tukio wakimzomea Polisi huyo.
 
Afande Bitrice aliyekuwa ndani akichukua maelezo ya Meneja wa Gest alivyosikia mzozo huo alitoka nje na kumfokea Polisi huyo huku akiniomba msamaha kwa kitendo hicho cha utovu wa nidhamu alichofanya Afande huyo.
 
Nikapokea msahama huo nikaokota picha ya Yesu iliyokuwa kwenye Rozari hiyo nikaiweka mfukuno huku Karanga za Rozari hiyo zikitapataa eneo hilo la Gest. 
 
Habari ya Mauaji hayo niliiripoti gazeti la Uwazi pamoja na Planet Redio kipindi cha Mcharuko wa Pwani
 
Mungu mkubwa baada muda nilipata taarifa kwamba Afande huyo aliyekata Rozari yangu amehamishwa.
 
Tukio la Pili ajari gari ndogo ilidaiwa kugonga Tren makutano ya Reli ya Kati barabara ya Mazimbu Jirani na Mataa ya lringa Road Majira ya saa 2 usiku.
 
Kama kawaida wadau wangu waliotapakaa kina mtaa boda boda wanaoegesha Pikipiki zao jirani kabisa na Reli hiyo eneo la Kiti moto walinipigia simu kunijuza tukio hilo.
Nilipofika eneo la tukio nilikuta polisi wakiendelea na kazi ya kuliondoa gari hilo lililonasa kwenye Kichwa cha Treni na kuburuzwa umbali wa takribani mita 100. 
 
Nikatimiza wajibu wangu wa kupiga Picha Polisi hao wakiendelea kulinyofoa gari hilo,chaajabu Polisi mmoja alinivamia na kuniamulu kufuta Picha akigoma kupigwa Picha na kutolewa kwenye magazeti na Luninga, nami niligoma kufuta Picha nikimueleza kama hataki kupihwa Picha basi aondoke eneo la tukio.
 
Kauli hiyo ilimchefua kavamia kamera akitaka kufuta Picha tukaanza kusukumana tukigombea kamera.
Katika Purukushani hiyo kiongozi wa Polisi aliyekuwa eneo hilo aliingilika kati na kumuamulu Polisi huyo akuichia kamera na kuniruhusu kuendelea na majukumu yangu.
 
Askari huyo alitii amri hiyo ya bosi wake akaiachia kamera, nilipoikagua nikashuhudia Betri haipo niliitafuta bila mafanikio kufuatia giza nene lillotanda eneo la tukio.
 
Nikamfuta Polisi huyo nikimtaka anilipe Betri hiyo aligoma, usiku huo huo nikampigia simu bosi wake wakati huo alikuwa RPC UrIcH Matei kwa sasa ni RPC wa Mkoa wa Mbeya. 
 
Awari RPC huyo alinipa Pole kwa kadhia hiyo huku akiniuliza kama Polisi huyo na mfahamu, nikamueleza simfahamu ila namatambua kwa namba yake ya Jeshi la Polisi iliyobandikwa kwenye sale zake za Jeshi nikamtajia namba hiyo.
 
“ Basi Shekidele kesho asubuhi njoo hapa ofisini kwangu tufanye kikao na Polisi huyo tujue shida ni nini”.
Asubuhi nikatinga kwenye kikao hicho kilichohudhuriwan na vigogo wengine wa Polisi akiwemo askari aliyenifanyia vulugu. 
 
Baada ya kukiri kufanya hivyo Polisi huyo aliamuliwa kunilipa Betri hiyo inayouzwa shilingi elfu 50, afande huyo aliomba kulipa Pesa hiyo baada ya wiki moja.
 
RPC Mtei alimtaka Polisi huyo kumkabidhi Pesa hizo Afande Aminieli aliyebeba nyota 2 begani ambapo baada ya wiki alinipigia simu na kunikabidhi pesa hiyo.
 
Baada ya kukabidhi kesho yake nipanda basi nikaenda Kariakoo Dar kununua Betri hiyo”.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...