Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, June 10, 2022

MKUU WA MKOA MORO ASHIRIKI MDAHALO WA WAANDISHI WA HABARI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.


























 

                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro ameshiriki Mdahalo ulioandaliwa na Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ ulioshirikisha Wadau wa habari kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa.
 
Mdahalo huo uliofanyika jana Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ulikuwa na lengo la kujadili Ulinzi na Usalama wa Mwandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro. 
 
Mkuu wa Mkoa Martin Shigela jana alikuwa na udhuru hivyo aliwakilishwa na Kaimu Katibu Tarawa Mkoa wa Morogoro Dk Rosalia Rwegasira, aliyefunguka kikao hicho, kilichohudhuriwa na Makamanda wa TAKUKURU. Polisi, Uhamiaji, Jeshi la Zima Moto na Uokoaji na wenyeji Wanachama wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro. 
 
Picha za Makamanda hao na Majina yao zipo Profaili la Mtandao huu chini ya habari hii wacheki.
 
Mara baada ya kufungua Kikao hicho kilichoanza Majira ya saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana, Mwakilishi huyo wa Mkuu wa Mkoa aliwataka Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro kuandika habari zenye lengo la kuvitangaza vivutio vya mkoa huo.
 
” Serikali ya Mkoa wa Morogoro inatambua umuhimu wa Waandishi wa habari ndio maana ziara zote za Mkuu wa Mkoa lazima Waandishi muwepo.
 
Hivyo tunaomba kupitia nyinyi mtangaze vivutio vilivyomo ndani ya mkoa wetu mfano Utalii, Madini,Kilimo na biashara”alisema Dr Rosalia.
 
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya alilitaka Jeshi la Polisi kutopuzia taarifa za vitisho wanavyopewa Waandishi wa habari
 
 Kwa Upande wao Makamanda wa Zima Moto. Uhamiaji na Takukuru waliahidi kushirikiana kwa karibu wa Waandishi wa habari kwa kuwaunga kwenye Group la Whatsp, kama walivyofanya wenzao wa Polisi ambao kwa muda mrefu wamewaunga kwenye Group Waandishi wa habari na wanapeana taarifa kupitia kwenye Group hilo.
 
Wengine waliofanya hivyo ni Uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wamewaunga Waandishi wa habari kwenye Group lao.
Katika mdahalo huo kila upande ulitoa duku duku lake kwa maana ya Makamanda wa Vyombo vya ulinzi na Usalama pamoja na Waandishi wa habari.
 
Kwenye kipengele hicho Mwandishi wa Mtandao huu alimjibu Kigogo wa Polisi aliyetoa duku duku lake juu ya habari hasi zinazoandikwa dhidi ya jeshi hilo. 
 
Mwandishi wa habari hizi naye alitoa duku duku lake kwa kueleza alivyogombana na Polisi kwenye Matukio kiasi cha kukatiwa Rozali, pia Mwandishi wa Mtandao huu alimjibu Kigogo huyo wa Polisi juu ya duku duku lake alilotoa kuhusiana na habari alizidai sio nzuri kwa jeshi lake.
 
Habari hiyo nzito itaruka hewani hivi punde hivyo usikose kutembelea Mtandao huu muda wote.


No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...