Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 12, 2022

YESU ALIYE KUHANI MKUU. WAEBRANIA 4-14-16



 

 


 

”Basi iwapo tunaye kuhani  mkuu aliyeingia katika mbingu,Yesu Mwana wa Mungu, na tuiyashike sana Maungano yake.

 

 Kwa kuwa hamna kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika Mambo yetu ya udhaifu,basi yeye alijaribiwa sawa sawa na sisi katika Mambo yote,bila kufanya dhambi.

 

 Basi na tukaribie kiti cha Neema kwa ujasiri. Ili tupewe Rehema na kupata Neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”Hilo ndilo neno letu la Leo June 12. Leo sitalichambua neno hilo lakini nafarijika kwamba ndani ya neno hilo la Mungu majina ya mabinti zangu wote wawili yametajwa.

 

Pichani kuhani Mkuu  Dunstan Shekidele akiwa na uzao zake, Rehema Dustan Shekidele[kushoto] na Neema Dunstan Shekidele.

 

Wakiketi kwenye kiti wakipata Neema na Rehema kutoka kwa kuhani Mkuu baba yao.

 

.Neno la leo linaendana na Majina ya mabinti  hao lfahamike Rehema jina lake lingine ni Tumaini.na yote yanatumika sawia.

No comments:

Post a Comment

MUNGU ANASEMA WATU WABAYA NI KAMA BAHARI ILIYOCHAFUTA,HUTOA TOPE NA TAKATAKA.

Dustan Shekidele akifanya mahojiano na Watumishi wa Mungu Askofu Jacob Ole Mameo wa KKKT Jimbo la Morogoro.   ......Shekidele akiungana kwen...