Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, June 18, 2022

MWANAMUZIKI MAARUFU WA JAHAZI MORDEN TAARAB AVUTA JIKO LA KITANGA.


 


             Na Dunstan Shekidele, Morogoro.
 
“ Hayawi hayawi yamekuwa,Mawifi Pigeni vigeregere na Mashemeji Pigeni Miruziiiii,Wenye Nongwa Nendeni Mkanunie kwenu,”
 
Mpiga Kinanda Maarufu nchini anayepiga kazi kundi Maarufu la Jahazi Morden Taarab linaloongongwa na Mfalme Mzee Yusuf, Ally Juma Mgomi Maarufu Ally J ljumaa iliyopita ameikacha timu dhaifu ya Makapera na kujiunga na timu Kabambe ya Wanandoa. 

Ally J Mzee wa harakati za Mtu Mweusi alifanya harakati zake mpaka Jijini Tanga na kufanikiwa kuopota mtoto Mkali wa Kitanga Bi. Amina Kassim Mgunya.
 
Baada ya kupata taarifa za Staa huyo kuvuta Jiko, Mwandishi wa habari hizi leo alimtwangia simu na kuzungumza naye juu ya jambo hilo la Kheri duniani na Mbinguni.
 
”Shekidele ni kweli ljumaa iliyopita June 10 nilifunga ndoa na mchumba’ngu kipenzi Mamsapu Amina nyumbani kwao Mtaa wa Mabawa Tanga Mjini” alisema ‘Ally J’ huku akiwa na furaha ya ndoa. 
 
Wakati bajeti ya juzi ya Serikali iliyosomwa vizuri na Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba, ikiongeza ushuru kwenye bidhaa ya Nywele bandi’Mawigi’ Shemeji yetu Amina hilo halimuhusu ana unywele wake halisia, Mwanamke nywele Bhana Uweke upara umefiwa?”
 
Mtandao huu unawapongeza wanandoa hao kwa kutekeleza lbada hiyo ya ndoa.
 
Pia Mtandao huu una Muomba Mwenyezi Mungu ailinde ndoa hiyo idumu mpaka kifo kitakapowatenganisha wote tuseme Amen.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...