Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, June 18, 2022

MICHUANO YA PLANET NDONDO CUP IMEZINDULIWA JANA KWA NJEMBA KUTAFUNA MAANDAZI 40, SODA NA MAJI.

Sehemu ya mashabiki waliofurika jna kwenye uwanja wa Saba saba nyomi hii imezunguka uwanja wote wa Saba saba
Karatasi za Majina ya wachezaji zikiwa na upunguvu wa majina ya pili


Alen Mwinyi Mpemba wa Chake chake kulia akiwa bize jana kutanga mtanange huo
Ni bao. Kipa wa Black People Peter Larbi akiruka bila mafaniko kuokoa mpira wa juu uliopigwa na winga wa Chadongo Calvin na kuipatia timu yake bao pekee kwenye mchezo huo.







 Mshambuliaji hatari wa Black People Mshasha ambaye kwa sasa anakipiga timu ya Singida Big Stars zamani DTB akiwa ni sehemu ya watu waliochangia kuipandisha ligi kuu timu hiyo akishika nafasi ya Pili kwa ufungaji kwenye timu hiyo akitambuliwa na Mlundi Hamisi Tambwe.







 

 

 

                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 

 MICHUANO ya Planet Ndondo Cup imezinduliwa jana kwenye Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa, kwa Jamaa Mmoja’Njemba’ Said Misosi Kutafuna Maandazi 40 akisukumia na Soda Moja  pamoja na Maji lita Moja na nusu.

 

 Michuano hiyo iliyoandaliwa na kituo cha Redio Planet cha Mkoani hapa imeshirikisha timu kali  zenye mashabiki kibao Mkoani Morogoro.

 

 

Timu hizo ni Black People Kutoka Mji Mpya, Black Viba kutoka Vibandani, Chadongo Fc kutoka Mafisa kwa Mambi, Wakushi Fc Kutoka Manzese ya Morogoro na Salange Fc kutoka Stend ya Mabasi Msamvu.

 

 

Katika mchezo wa Uzinduzi uliopigwa jana na kutangazwa Live na Mtangazaji Mahiri wa Mpira Mkoani Morogoro Alen Mwingi’ Mpemba wa Chake chake,’ Chadongo iliwanyuka wapinzana wao wakubwa Black People  bao1-0.

 

 

Bao hilo pekee lililoitupa nje ya michuano hiyo inayoendeshwa kwa mfumo wa Mtoano ‘Ngumi Jiwe’ limefungwa na Calvin aliyetajwa kwa  jina Moja kwenye Orodha ya Majina ya wachezaji ambayo Mwandishi wa Mtandao huu amepewa na Waandaji kama inavyoonekana Pichani.

 

 Huu ni udhaifu kwa mashindano makubwa kama hayo badhi ya wachezaji kuorodheshwa kwa jina Moja, hali hiyo hutoa usumbufu kwa Waandishi wa habari kwenye lshu ya kuripoti hasa ukizingatia mchezo huo ulikuwa ukitangazawa live na Mtangazaji  akitumia karatasi hizo zenye majina moja moja.

 

Mfano ikitokea ishu ya kukata rufaa mara nyingi kamati ya mashindano huwatambua wachezaji kwa Majina kamili yaliyoorodheshwa kwenye karatasi hizo Pia Waamuzi wanapotoa adhabu ya kadi nao hutumia karatasi hizo kwenye ripoti zao zinazokwenda kwenye kamati ya Mashindano.

 

 

Kwa vile Mwandishi wa Mtandao huu nawafahamu wachezaji wengi wa mkoa wa Morogoro hilo halikumpa shida sana alitumia uzowefu wake kuwatambua wachezaji hao.

 

 

Ukiondoa kasoro hiyo uzinduzi wa michuano hiyo umefana sana ambapo kundi la mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo kwa kiingilio cha elfu 2 kila shabiki alilipa kingilio hicho alipewa zawadi ya Peti Moja ya Pilau.

 

 

Wakiwa ndani unagonga Pilau hilo mashabiki hao uliburudishwa na Muziki Mnene kutoka kwa Dj Andrew B.

 

 Kama kawaida Mwandishi wa Mtandao huu amekusanya matukio kibao zikiwemo Picha za Njema huyo akifakamia maandazi hayo 40 hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...