Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MREJESHO. Juzi Mtandao Pendwa wa Shekidele uliripoti habari ya ndege aina ya Utongwa Kisiesie wa Kijani aliyejenga kiota chake kwa kushirikiana na mume wake kwenye moja ya taa za Ulinzi za nje ya nyumba.
Walipomaliza ujenzi ndege hao walitanga mayai mawili na June mosi walianza kuyahatamia, ilipofika usiku taa hizo zilipowashwa huku ndege huyo akiwa kwenye jukumu lake la uzazi kwa maana ya kuyahatamia mayai hayo ambayo baada ya siku kadhaa yangempatia watoto’Makinda’ aliunguzwa na joto kali la taa hiyo iliyowaka usiku kucha.
Baada ya kuunguzwa na joto kali la taa hiyo Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia ndege huyo akihangaika mara anatoka kwenye kiota hicho mara anaingia tena kuyahatamia mayai yake.
Paparazi wa Mtandao huu alipomuona ndege huyo akihangaika alipofanya uchunguzi wa haraka na kugundua tukio hilo alimtwanga Picha na kurusha habari hiyo kwenye Mtandao huu na kuahidi kufuatilia tukio hilo mpaka mwisho kujua kama Mayai hayo yatawia kwa kukosa kuhatamiwa[Joto la ndege huyo] usiku kucha ama joto kali la taa hiyo litakuwa mbadala wa joto la ndege huyo na Mayai hayo kuanguliwa na kutoa makinda?.
Habari zikufikie Mpendwa msomaji wa Mtandao wa shekidele kwamba kulipokucha kwa maana ya siku iliyofuata asubuhi na mapema ndege hao Mke na Mume walibeba mayai yao na kuhama kwenye taa hiyo.
June 2 Mwandishi wa Mtandao huu alipofanya uchunguzi hakuwaona ndege hao, alipoamua kusafiri hadi kwenye paa la nyumba eneo ilipo taa hiyo kwa kutumia usafiri wa ngazi,alipofika alikuta patupu hakumuona ndege wala Mayai.
Swali je ndege hao walitumia mbinu na njia gani kuhamisha mayai hayo, waliyabeba kwa mdomo au kwa miguu yao? Uchunguzi wa stori hiyo ya kitaa umefika tamani kwa kukuacha na maswali hayo 2.
No comments:
Post a Comment