Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 5, 2022

JUMBE WA NENO LA MUNGU.KUTOKA WAGALATIA 6-9







 


WAGALATIA 6-9 

Na Mtumishi Dunstan Shekidele,Morogoro

“Tena tusichoke katika kutenda Mema, Maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho”Hilo ndilo neno letu la  Jumapili ya Leo June 5.

 

 Neno hili linatukumbusha kutenda Mambo Mema kwa maana ya kuwasaidia wenzetu wenye uhitaji wa namna yoyote ile.

 

 Mungu kupitia Vitabu vya dini amesema “Mtu nayemsaidia Mja wangu amenikopesha nami nitamlipa mara dufu.”

 

 Kumbe basi tunakumbushwa kutenda mame kwa kujiwekea hazina ya kesho yetu, Kunafaida gani unasaka mali kwa jasho na damu unajilimbikizia mali unakula wewe na familia yako tu hujali Masikini wala Majirani zako, pengine ubize huo wa kusaka Mali hata kwenye lbada ya kumuomba Mungu aliyekupa hizo Mali huna.

 

 lfahamike kusaka mali au kuwa tajiri sio dhambi lshu ni kwamba  hiyo mali unaitumiaje,unakumbuka kuwasaidi wenye uhitaji? Pili unamtolea Mungu fungu la 10? Kwa maana ya kuwasaidi Watoto Yatima, Wajane, Walemavu na kumjengea Mungu nyumba ya lbada?Majibu ya Maswali haya unayo wewe Mwenyewe.

 

Hii naina maana kwa matajiri peke yake hata wewe unayesoma habari hii  hicho kidogo ulichonacho unawakumbuka wenzio wenye uhitaji, hizo nguo za watoto zao zinazowabana uliwahi kuzipeleka kwa watoto yatima, jirani yako kalala njaa wewe unakiloba cha unga ulimpunguzia hata kilo moja?

 

 Sote tumashahidi kuna baadhi ya Matajiri wamekufa na kuuacha utajiri wao wamekwenda na kitu kimoja tu roho yake, kwa sasa watu wengine wanautumia huo utajiri wake wakati watakavyo ili hali Mwenye huo utajiri yuko mbele za Mungu akisubiri hukumu.

 

 Aidha hakuna mtu aliyefirisika kwa kumsaidia mtu mwenye uhitaji, hasara roho Pesa  Makaratasi, kuna maisha mengine baada ya haya ya hapa chini ya Jua.

Kwa leo Mtumishi wenu naweka nukta hapa Mungu akipenda tukutane Jumapili ijayo kwa somo lingine.

 

 Pichani Mwandishi wa habari hizi ambaye ni Mtoto wa Mkuliama mwenye maisha ya kawaida kabisa kidogo alichopata akigawana na watu mbali mbali wenye uhitaji wakiwemo Watoto Yatima, Walemavu, na Wagonjwa wodini

 

 

. Pia alitumia sehemu ya kazi yake ya Uwandishi wa habari kusaidia watu wenye uhitaji mbali mbali kupitia Magazeti Redio na Mtandao huu.  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...