Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 19, 2022

MCHEZAJI ALIYEBAMIZA KICHWA UWANJANI AZUA MSTUKO DAKTAR AKIMBILIA KUMNYOFOA ULIMI.

Cheki show hii, Mshambuliaji wa Chadongo Fc Hassan Mkoata Messi wa Chamwino kushoto akigombea mpira wa juu na beki wa  Black People Salim Mbonde kwa staili ya kumsukuma
....Mbonde akienda Chini, baada ya kulishwa dona la Messi wa Mji Kasoro bahari
.... Mbonde akipiga chini Kichwa, huku Messi akinyoosha mikono la kulalamika baada ya refa kupiga filimbi ya adhabu
                                   ....Mbonnde kazima
...Wachezaji wenzie akiwemo Feisal Yassin aliyeinama wakimtikisa bila mafanikio
                              .....Daktari kaingia uwanjani

Daktar Lucas akihangaika kunyofoa ulimi wa mchezaji huyo

 

                    Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 BEKI kisiki wa timu ya Black People Salim Mbonde, Juzi alizua taharuki kwa dakika kadhaa baada ya kusukumwa na Mshambuliaji wa Chadongo Fc Hassan Mkota’Messi wa Chamwino’ na kuangukia Paji la uso.

 

  Chanzo cha tukio hilo lililonaswa hatua kwa hatua na Mpiga Picha Mzowefu wa Mtandao huu, bei huyo wakati akigombea mpira wa juu ulioelekezwa langoni mwake akiwa hewani alisukumwa na Mshambuliaji wa Chadongo Hassan Mkota ‘Messi wa Chamwino Moro’alikosa balance akaanguka na kubamiza kichwa kwenye uwanja Mkavu wa  Saba saba,Unaomilikiwa na Umoja wa Vijana wa CCM’UVCCM’.

 

 Baada ya kutua chini ‘alizima’ hakutikisika hali hiyo ilimsukuma  Mwamuzi wa mchezo huo wa nusu fainali ya Michuano ya Planet Ndondo Cup, Fikiri Magari kumwalika Daktari  Lucas.

 

Dkt Lucas alivyoingia Uwanjani kitu cha kwanza alikimbilia kudaka ulimi wa mchezaji huyo usitumbukie ndani,huku akiwaamulu wachezaji wengine kumvua viatu kwa lengo la kuilekeza mishipa ya fahamu na ile ya Mapigo ya Moyo.

 

 

Mungu ni Mwema baada ya huduma hiyo ya kwanza mchezaji huyo alizinduka na kuendelea na mchezo huo uliotamatika kwa Taifa  hilo la Watu Weusi’Black People’  kutoka Mji Mpya kutupwa nje ya Michuano hiyo baada ya kuchapwa bao 1-0 na Chadongo Fc.

 

 

Nusu fainali ya Pili ya Michuano hiyo itapigwa ljumaa hii kwenye uwanja huo huo wa Saba saba Kati ya wapinzani wa jadi, Black Viba yenye maskani yake Vipandani Kata ya Mbuyuni na Wakushi Fc yenye Maskani yake Manzese Kata ya Mafiga kata hizi mbili ni Majirani zinatenganishwa na barabara ya SUA.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...