Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, June 21, 2022

HII KALI , MUME ACHWA NA MKEWE KWA TABIA YAKE YA LA KULA KILO 2 ZA WALI KILA SIKU.

Saidi Misosi akiendelea kufakamia maandazi 4o soda na Maji
.........Kazi ikiendelea huku akikodolea machozi umati wawatu unamshangaa


 


                           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 Wakati kwa sasa ndoa nyingi zinavunjika huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni usaliti, hali hiyo imefika mbali zaidi kwa siku za hivi karibu ambapo baadhi ya wana ndoa wamefika hatua ya kuwana kwa kupigana risasi  kisa eti ni kwa nini hakupokea simu zaidi ya mara kadhaa.

 

 

Mic Call 4 ukirudi nyumbani unatandikwa risasi 4 kila Mic Call Moja Risasi Moja, hii sio Sawa tukumbuke kuna Maisha Mengine baada ya Mapenzi [Ndoa].  

Hali hiyo imekuwa tofauti kwa bwana Said Misosi yeye ameachwa na mkewe kwa kile alichodai kula sana ambapo kwa siku anakula kilo mbili za Wali peke yake.

 

 

Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Michuano ya Planet Ndondo Cup ljumaa iliyopita ndani ya Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa Said Misosi alisema.

 

” Leo  hapa uwanjani ni kama nimeonja nimekula maandazi 40 Soda moja na Maji lita Moja na nusu. Uhalisi kwa siku nakula kilo 2 za Wali, hali hiyo imepeleka mke wangu kunikimbia kutokana na hali hiyo kwa sasa niko msela sihitaji tena mwanamke.

 

 Ninachofanya namwita Mwanamke ananipikia namlipa chake anasepa zake, namshukuru Mungu nimeshinda mashindano mengi ya kula juzikati kwenye shindano ya Tonge Nyama pale msamvu nimeshinda baada ya kula kila 2 za Wali na Kuku wawili”alisema Said na kuongeza.

 

 

“Namshukuru Mungu mashindano haya ya kula yamenipa umaarufu na Pesa zilizopelekea kujenga Nyumba maeneo ya Lukobe pia namiliki Boda boda 2”alisema mbabe huyo wa Mankuli.

 

 

Alipoulizwa sababu za yeye kula chakula kingine kwa wakati mmoja zinatokana na nini? Alijibu.

”Nikwenda hospital kucheki  baada ya kunipima Madaktari walisema  ninakina kirefu cha mfuko wa kuhifadhi chakula hivyo napaswa kula chakula kingi”alisema Said mwenye uzito wa Kilo 72.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...