Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, June 4, 2022

HII INAWEZA KUWA STORI YA KITUKO CHA USWAZI.



 


                     Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Nikiwa mitaa ya home Majira ya usiku Mei 28 niliwashuhudia ndege wawili jike na dume aina ya Kisiesi wa kijana wakishirikiana kujenga kiota chao kwenye moja ya taa za ulinzi za nje ya nyumba zenye mfano wa bakuli.

 

Nafsi moja alinituma niwafukuze nikihisi kiota hicho kinaweza kufifisha mwanga wa taa hiyo, lakini nafsi  nyingine iliyojaa matendo ya huruma ikanielekeze niwaache viumbe hao waendelee na kazi ya kujenga nyumba yao ndani ya taa hii.

 

Katika mvutano wa nafsi hizo mbili hatimaye nafsi ya matendo ya huruma iliishinda hivyo nikawaacha ndege hao kuendelea na ujezi wa mjengo wao waliyoukamilika kwa siku mbili.

 

Mei 30 mpaka mei 31 walitaga mawai mawili na June Mosi walianza kuyalalia’Kuyahatamia’.

 

 Siku hiyo majira ya saa 3 usiku niliporeja nyumbani nikitokea kazini baada ya kuoga  nilitoka nje nikapunzika eneo la bustani  nikiwa na vazi la bukta na Singlend ‘Fest’ huku nikiwa na kikombe cha kahawa nikipunga upepo nikitafakari changamoto za haya maisha yaliyojaa tabu, raha na usaliti.

 

Ghafra nikamuona ndege huyo ameacha kuhatamia Mayai  yake ametoka nje akiruka ruka huku akipiga kelele, nikaweka chini kikombe cha Kahawa nikaingia chumbani nikachukua Kamera nikaseti tarehe na saa kama picha inavyoonyesha June 1 saa 3 na dakika 48.

 

 Nikasogea eneo la tukio kuchunguza chanzo cha ndege huyo kukurupuka kwenye nyumba yake usiku mnene nikamngwanga Picha, baada ya dakika 3 hivi karejea tena kwenye kiota chake na kuendelea kuyahatamia Mayai yake.

 

Dakika 4 baadae katoka tena na kuendelea kupiga kelele, nikasogea tena kujua tatizo ni nini, nilipochunguza nikabaini  Ndege huyo anaunguzwa na Joto la taa hiyo.

 

Hivyo hadi naingia ndani kulala majira ya saa 4 na nusu usiku ndege huyo kama alivyo mzazi yoyote mwenye mapenzi  na wanae alikuwa akifanya hivyo dakika 3 anaingia kwenye kiota kutimiza majukumu yake ya ulezi na dakika 3 akiunguzwa anacha jukumu hilo na kutoka mbio huku akilia kwa uchungu wa kuunguzwa na taa na ule wa kuacha jukumu lake la ulezi wa kuhatamia Mayai yake.

 

Baade nikawa na maswali mengi juu ya tukio hilo swali la kwanza je mayai hayo kutolaliwa usiku mzima hayawezi kuvia’kwa maana ya kuharibika?

 Swali la Pili japo mayai hayo hayakulaliwa ipasavyo kwa maana ya kupata joto la ndege huyo je joto la taa hiyo haliweze kuwa mbadala wa joto la ndege huyo?.

 

 Nalifuatilia tukio hili Mpaka mwisho hivyo tusubiri kuona mwisho wa tukio hili itakuwaje mayai hayo yatavia au yatatotolewa na kutoa makinda ya ndege?endelea kuwa jirani na Mtandao huu kupata majawabu ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...