Mnenguaji wa Maisha Mpaya Husma Bongo akiiga Style ya Sakho ya Kunyunyiza
Wanengauji wa Maisha Mapya Kutoka Kushoto Husna Bongo Kavrlla JohnKati] na Amida Paganisha kwa pamoja wakinyunyiza
Mayele wa tatu kutoka kushoto akipiga mkono mara tatu kabla ya kutetena baada ya kufunga bao,
huku akisindikizwa na baadhi ya wachezaji wenzake na kocha wa Viungo wa Yanga wa kwanza kushoto
....Wakitetema na kumwaga mtetemo huo kw akichwa
Na Mlala Nnje Dunstan Shekidele,Morogoro.
KWA sasa moja ya Vionjo vya Ligi kuu ya Tanzania Bara inayoelekea ukingoni ni Staili za Ushangiliaji za wachezaji wa kigeni wa timu kongwe nchini Simba na Yanga.
Style za wachezaji hao Fiston Kalala Mayele Mkongomani raia wa Congo anaye kipiga Yanga ambapo kila akifunga bao anakimbilia kwa mashabiki na kupiga mikono yake mara tatu kisha anatetema.
Naye Mshambuliaji wa Simba Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal yeye akifunga bao hukimbilia kwa mashabiki na kuonyesha ishara ya kunyunyiza ubani.
Style za Wachezaji hao kwa sasa zimewaingia Mashabiki wa timu hizo kongwe nchini.
ljumaa iliyopita Mlala Nnje wa Mtandao huu akiwa kwenye Pilikapiliza zake za kusaka matukio kwenye kumbi mbali mbali za burudani Mkoani Morogoro aliwashuhudia wanenguaji nyota wa Band Pendwa ya Maisha Mapya, Husna Ramadhani Maarufu Husna Bongo, [Kushoto] Kavella John [Kati] na Amida Paganisha, wakinengua kwa style za Wachezaji hao.
Ubunifu huo uliwapatia pesa wanenguaji hao ambapo Mashabiki wa Simba na Yanga waliokuwepo ukumbini hapo wakila raha,waligombea kupanda jukwaani kuwatunza wanenguaji hao pale walipocheza Style za Mchezaji wa timu yao.
Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mlala Nnje ulionyesha Mashabiki wa Style ya Mayele waliongoza kuwamwangia pesa nyingi wanenguaji hao.
No comments:
Post a Comment