YEREMIA 17-9
“Moyo huwa Mdanganyifu kulilko Vitu vyote,unaogonjwa wa kufisha, nani awezaye kuujua?.
Mimi BWANA, nauchunguza Moyo,navijaribu viuno,hata kumpa kila Mtu kiasi cha njia zake,kiasi cha Matunda ya Matendo yake.
Kama kware akusanyaye Makinda asiyoyazaa,ndivyo alivyo Mtu ajipatiaye Mali,wala si kwa haki,katikati ya siku zake zitaachana naye, na Mwisho wake atakuwa Mpumbavu” Hilo ndilo neneo letu la leo Jumapili ya Mei 22.
Neno ambalo linatukumbusha kuacha dhuruma likitusihi tusikubali kudanganywa na moyo kwamba tudhurumu watu ili tupate Mali ambazo mwisho wa siku tunakufa na kuziacha hapa hapa duniani na kwenda kuhukumia kesho mbele za Mungu maneno hayo yanasema mwisho huo ni wa utumbavu.
Kumbe basi tunakumbushwa kutokubali kudanganywa na Moyo wa tama ili mwsiho wetu uwe mzuri tuingie kwenye Pepo ya Mwenyezi Mungu.
Tusikubali kudanganywa na Moyo kuchukua kitu chochote kisicho kuwa mali yako, kwenye neneo hilo Mungu ametolea mfano wa Kware ambaye amekubali kudanganywa na Moyo ukamtuma achukue Makinda ambayo hakuya zaa yeye.
Mzazi aliyeingia Reba na kuza makinda hayo alitoka kwenye kiota chake kwenda kuwatafutia Chakula watoto zake.
Aliporejea na Chakula amekuta Makinda yake hayapo yameibiwana Kware.
lnauma sana amebaki na hudhuni huku akiwa na chakula chake mdomoni.
No comments:
Post a Comment