Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 23, 2022

KUMBUKIZI YA MSANII MANGWEHA



 

.

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Du Miaka inasonga.

 Jumamosi ya Mei 28 aliyekuwa Msanii Maarufu nchini wa Muziki wa Kizazi Kipya Albert Keneth Mangweha Maarufu ‘Ngweha’ anatimiza Miaka 9 toka alipofariki dunia.

 

Msanii huyo Mkazi wa Kihonda Mtaa wa Mazimbu Road Mkoani hapa, alifariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini na maiti yake kurejea nchini na kuzikwa katika Makaburi yaliyopo nje ya Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Parokia ya Mt Monica Kihonda.

    

Imeelezwa kwamba umati mkubwa wawatu uliofurika kwenye mazishi ya Magweha yamevunja rekodi Mkoani Morogoro, Mwandishi wa habari hizi aliyeshiriki Mazishi hayo Mwanzo Mwisho naye amethibitisha hilo.

 

 

 Jumamosi ya wiki hii Mei 28  familia ya Msanii huyo kupitia Mama yake Mzazi Bi Denisia Mangweha Mkazi wa Kihonda Mazimbo Road ambaye ni mmoja wa Vigogo wa Kanisa la Mt Monica Kihonda kwa kushirikiana na wasanii wa Muziki wa kizazi Kipya nchini wakiongozwa na rafiki Mkubwa wa Marehemu Mangweha Hamza Mgaza Maarufu’M 2

THE P’ watatinga kwenye kaburi la Mangweha na kufanya lbada ya Kumuombea sambamba na Kuchoma Mishumaa Mwandishi wa Mtandao huu atashiriki kwenye ibada hiyo.

 

Kuanza leo Mpaka Jumamosi Kila siku Mtandao huu utarusha habari na matukio ya mzishi ya Msanii huyo pamoja na Picha ya Mchumba’ke ambaye ni Mzungu Raia wa Uingereza.

 

 

Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote, Pichani Mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye kaburi la Mangweha  Mei- 29- 2020 Mara baada ya kukamilika kwa lbada ya Maombi ya Marehemu huyo.  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...