Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, May 21, 2022

MSHAMBULIAJI APIGA 3 APEWA MPIRA KISHA ANYANG’ANYWA.



 
                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
 UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona ya Filahuni.
 
Msemo huu umetimia mkoani hapa,baada ya Mshumbuliaji hatari wa Kikosi cha Pili cha Maafande wa Ruvu Shooting Said 
 
Hamis’Kunguru’ kufunga bao 3 na kupewa mpira kama sheria ya soka inavyoelekeza kabla ya sheria hiyo kuvunjwa kwa mchezaji huyo kunyang’anya Mpira huo na Mwamuzi’Refa’.akiambulia kupiga nao Picha tu.
 
Tukio hilo la aina yake limetokea juzi kwenye Mashindano ya Kijana chini ya Miaka 20 yaliyoandaliwa na Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA.yanayoendelea Uwanja wa Saba Saba wakitii maelekezo ya shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF.’
 
TFF iliviangiza vyama vyote vya soka nchini kuanda michuano ya Vijana na Soka la Wanawake kwenye maeno yao.
 
Mwishoni mwa mwezi uliopita MDFA uliandaa michuano hiyo na kushirikisha timu za Vijana Under 20 zaidi ya 20 huku timu 3 kutoka wilaya nyingine zikiomba kushiriki michuano hiyo.
 
Timu hizo ni Kilombero Soccer Net Kutoma Wilaya ya Kilombero, Ruvu Shooting na Pwani Soccer Fondation kutoka wilaya za Mkoa wa Pwani. 
 
Juzi Ruvu Shooting ilitinga hatua ya Pili ya Michuanio hiyo kwa kishindo baada ya Kuindandika bila huruma Kilakala Academy bao 6-0 huku mabao yote yakipatikana kipindi cha Pili baada ya timu hizo kwenda sare dakika 45 za awari.
 
Mabao ya washindi yalifungwa na Sylvester Otto aliyefunga bao 1. Haruna Hamis aliyefunga bao 2 na Said Hamis’Kunguru’ aliyefunga bao 3 ‘Hat Trick’. 
 
Kwa Mujibu wa sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia’FIFA’ Mchezaji akifunga bao 3 kwenye mchezo mmoja Mwamuzi wa mchezo anapaswa kumkabidhi mpira mara baada ya gemu husika kukamilika. 
 
Hivyo baada ya gemu hiyo kukamilika Kunguru aliyejiunga na Ruvu akitokea Chamwino Youth ya Morogoro alimfuata Mwamuzi wa mchezo huyo Rackson James kwa lengo la kukabidhiwa Mpira wake kama sheria inavyoelekeza. 
 
Refa huyo aligoma kumkabidhi Mpira kwa madai kwamba Mpira huo sio wa chama cha Soka bali ni watimu pinzania ya Kilakala hivyo hivyo asingeweza kumkabidhi mpira wawatu. 
 
Baada ya kuelezwa hivyo Mchezaji huo aliamua kumwita Mwandishi wa Mtandao huu na kumuomba refa huyo amkabidhi mpira huo kwa ‘Bosheni’ ili apige nao picha kwa lengo la kuweka kukumbuku kwenye maisha yake ya Soka.
 
”Shekidele Picha zangu utanitumia WatSsap”alisema Said Hamis’Kunguru’ ambaye kesho habari zake ya kutoka dini ya kiislamu na kujiunga na dini ya Kkristo zitaruka hewani.
Angalia Picha  zaidi za tukio hilo kwenye Facebook  shekideleMkude Simba mchezaji huyo akionyesha hudhuni baada ya kukosa haki yake ya Msingi ya kukabidhiwa mpira huo.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...