Kikosi cha Chamwino Youth
Nyumbani ni nyumbani asiyekumbuka kwao ni mtumwa.
Mara baada ya gemu ya Ruvu na Chamwino Youth kutamatika kwenye michuano ya Vijana chini ya Miaka 20 inayoendelea uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro,
Mshambuliaji hatari wa Ruvu Said Hamis ambaye aliuzwa na Chamwino kwenda timu hiyo kikosi cha Pili cha Wajeda wa Ruvu Shooting. alikwenda kwenye bechi la timu yake hiyo ya zamani na kumsalimia Kocha wake Juma Mgonja[Pichani Kulia kisha akawapa ‘Hi’ kubwa wachezaji wenzake kama anavyonekan Pichani.
Kwenye gemu hiyo Chamino alibugizwa bao 5-0 huku Said alifunga bao 1 na kupika mabao 2 kwa maana ya kutoa pasi za mwisho'Assit'
TALENT.
Vijana wa Chamwino kama wana sumaku Vile check wanavyonasa mipira.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Wakati Ruvu Shooting wakijianda kukipiga na Yanga kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, Vijana wao wa Kikosi cha Pili ‘Ruvu Shooting Under Twenty’ juzi walitoa onyo Kali kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi ya Vijana chini ya Miaka 20 inayoendelea Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.
Kikosi hicho cha Pili cha Ruvu juzi kilianza michuano hiyo kwa kishindo baada ya kuinyuka timu ngumu ya Chamwino Youth ya Mkoani hapa kwa kuibugiza mabao 5-0 na kupeleka salam kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo. Vijana hao wa Ruvu wenye makani yao Ruvu Mlandizi Mkoani Pwani waliutawara mchezo huo kwa muda wote wa dakika 90.
Licha ya kufungwa mabao hayo 5 lakini Vijana wa Chamwino wanaonolewa na Kocha Maarufu Mkoani Morogoro Juma Mgonja’Mpale kutoka Same’ walionyesha Upinzani Mkali huku makosa mengi ya Kipa wao ndio yaliopelekea kubugizwa lundo hilo la mabao.Sehemu kubwa ya wachezaji wa Ruvu wametokea Mkoaniu Morogoro ambapo Mwandishi wa habari hizi aliwashuhudai wachezaji kadhaa kutoka Morogoro wakiwa na timu hiyo.
Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Said Hamis aliyetokea Chamwino Youth, Calvin aliyetokea Changarawe ya Mzumbe Moses aliyetokea Black Viba na Sepepa aliyetokea Black People ya Mji Mpya.
KWA NINI RUVU NA YANGA WANACHE KIGOMA.
Kwenye moja ya kanunu za TFF zinaruhusu timu yoyote kuchagua uwanja wowote Tanzania bara kwenye michezo yao 2 ya ligi kuu.
Hivyo Wanajeshi hao wa Ruvu ambao ndio wenyeji wa Yanga waliamua kumpeleka Mayele Kigoma akale Migebuka kwenye kwenye gemu yao itakayopigwa kesho saa jioni uwanja wa Lake Tanganyika.
Wachambuzi wa Mambo wanadai kwamba pamoja na mambo mengine Majeda hao wa Jeshi la Kujenga Taifa’JKT’ Ruvu wamelenga kuvuna mapato kwenye gemu hiyo. lkumbukwe KMC iliwapeleka Simba Tabora ambapo umati wamashabiki ulifurika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kumshuhudia Mwamba Bernard Morrison akiupanda Mpira na kusababisha watoza ushuru hao wa Kinondoni Dar kuvuna mkwanja mrefu licha ya kuambulia kichapo cha bao 3-1 kwenye gemu hiyo.
No comments:
Post a Comment