Mbwiga Mbwiguke 'Mkole wa nyani Mkia' akiwapa Hi wachezaji na benchi la Ufundi la Ruvu Shooting
...Mbwiga akielekea Jukwaani kupiga stori na masela
...Mbwiga kulia akiwa na Kikosi cha Black Viba kinachotarajia kushiriki michuano ya Ndondo Cup Dar
Mbwiga akiwa na masela jukwaani
.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro
MAANDALIZI ya Michuano pendwa ya Ndondo Cup yaliyoandaliwa na Clouds Media yanazidi kushika kasi ambapo Mtangazaji Mwenye maneno Mengi wa Kipindi cha Michezo Clouds Fm ‘Mzarumo’ Gwiga Mbwiguke jana ametinga Kata ya Mbuyuni Mtaa wa Vibandani na kuzungumza na Uongozi wa timu ya Black Viba inayoshiriki Michuano.
Mara baada ya kuzungumza na Uongozi, Wachezaji na mashabiki wa Viba, Majira ya saa 10 jioni jana hiyo hiyo Mbwiga alitinga uwanja wa Saba saba kushuhudi timu hiyo ya Viba inayoshiriki Ligi ya Vijana chini ya Miaka 20’Under Twenty’ akikipiga na Wanajeshi wa Ruvu Shooting.
Mbwiga alipotinga Uwanja hapo alipomuona Mwandishi wa Mtandao huu aliangua kicheko na baada ya wawili hao kusalimiana Mbwiga alisema.
” Shekidele nisindikize kwenye mabenchi ya timu zote mbili nikawasalimie unajua tena sisi ni wanamichezo”.
Mwandishi wa Mtandao huu alikubali Ombi hilo wakaanzia timu ya Ruvu, wakaja Black Viba’ambayo ni timu pekee kutoka Moro Inayoshiriki Ndondo Cup na kupiga nayo Picha baada ya kutoka hapo Mzaramo huyo alipanda jukwaani na kuimba nyimbo za Ndondo Cup na Mashabiki wanaozaniwa kuwa wa Black Viba.
Clip Video za tukio hilo la nyimbo hizo za Mbwiga na mshabiki zitaruka hewani hivi Punde Shekidele Online Tv.
Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Black Viba lman Masoud alisema
”Shekidele sisi tumeingia ndondo Cup ndio maana umeona Mbwiga kaja Maskani kwetu mchana na jioni hii kaja Saba saba, tutakwenda Dar kutoa upinzani hawa Vijana wetu wa Under 20 wanaosumbua kwenye michuano hiii ya Jina tutawachanganya na kaka zao mafundi wa Mpira timu tumeisuka haswa.
Si unajua Moro imejaa Vipaji kwa faida ya wasomaji wa Mtandao wa Shekidele kwenye michuano hiyo hatuta tumia jina letu la Black Viba tutatumia jina la Moro Town Fc, tunaomba Waluguru wanaoishi Dar waje uwanjani kutusapoti”alisema Kiongozi huyo.
Katika gemu ya jana Vijana wa Viba Under 20 walitoka sare ya bao 1-1 na Vijana wa Ruvu Under 20. Gemu hiyo ilikuw ana ushindani mkali kufuatia ubora wa timu zote mbili. Viba waliotawara mchezo dakika 45 za kwanza walikwenda mapunziko wakiw ambele kwa bao 1, huku Vijana wa Ruvu wanaonolewa na kocha Rahim Madega wakitawara kipindi cha Pili na kufanikiwa kusawazisha bao hilo baada ya Vijana wa Viba kukata moto kipindi hicho cha Pili.
Picha za matukio ya gemu hiyo zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment