Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 24, 2022

MWENDELEZO WA KUMBUKIZI YA KIFO CHA MSANII MANGWEHA.

 

 

Na Dunstan Shekidele.Morogoro.

 

 

Leo ni siku ya tatu Mtandao Pendwa wa Shekidele unaendelea kukuletea matukio ya kumbukizi ya Miaka 9 ya Kifo cha  Msanii Maarufu wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini  Alibert Kenneth Mangweha ’Ngwea’.

 

Hivyo kuanzia Juzi Jumatatu Mpaka siku ya Kilele cha kumbukizi  ya kifo cha Mpendwa wetu Jumamosi Mei 28 wiki yote hii Mtandao huu utarusha matukio ya Kumbukizi cha kifo cha Msanii huyo Mwana ‘Mo Town’ aliyefariki dunia Mei 28-2013 nchini Afrika Kusini na kuzikwa hapa nyumbani kwao Morogoro.

 

Leo Mtandao huu anaendelea kushurusha matukio hayo kwa picha ya Mchumba wa Marehemu Ngweha  Misheli raia wa Uingereza[Kati] ni Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt Monica Kihonda Padri Msimbe na kulia ni Msanii Maarufu wa Muziki wa Kizazi Kipya Hamza Mganga Maarufu ‘M 2 THE P’ ambaye ni rafiki Mkubwa wa Marehemu Mangweha.

 

Watatu hao walipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu mara baada ya lbada ya Kumbukizi ya Mwaka 1 wa kifo cha  Mngweha Mei 28 -2014.

 

lbada hiyo iliyosheheni Mastaa Kibao wa hapa Tanzania ilifanyika nyumbani kwa Bi Denisia Mangweha ambaye ni Mama Mzazi wa Marehemu Ngwea.

 

Akijibu Maswali mbali mbali ya Mwandishi wa habari hizi likiwemo  la mchumba huyo wa Marehemu Ngwea Mama  Mangweha alijibu.

 

”Kweli huyu Mzungu ni Mkwe wangu mchumba wa Albert kabla ya Mwanangu Kufa alikuja kumtamburisha hapa nyumbani hivyo kama familia tunamtambua ndio maana umeona naye amekuja kushiriki  lbada ya  Maombezi ya Mwaka 1 wa Kifo cha Mume wake Mteule”alisema Bi Mkubwa huyo Mjane ambaye Mpendwa Mume wake Mzee Kenneth Mangweha naye alifariki dunia miaka kadhaa iliyopita.

 Katika kuthibitisha Maneno ya Bi Mkubwa huyo Mwandishi wa Mtandao huu alimshuhudia Mrembo huyo wa kizungu  akiwa ndani ya vazi la  rangi ya damu ya Mzee akimeremeta sawia na mawifi zake pamoja na Mama mkwe wake ambapo wote walipendeza na sare hiyo.

 

Tukutane kesho kwa habari nyingine ya kumbukizi ya matukio ya Kifo cha ‘Ngwea’

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...