Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 24, 2022

KUMBUKIZI KIFO CHA MANGWEHA. MAMA ANGUA KILIO AKIWA NA PICHA YA MAREHEMU MWANAE.



 


 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Bi Denisia Mangweha, ambaye ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini Marehemu Albart Mangweha’Ngwea’ ameangua kilio baada ya kuona Picha  Kumbwa ya Mpendwa Mwanae.

 

Mara kwa Mara Mwandishi wa  habari hizi alikuwa akitinga nyumbani Kwa Bi Mkubwa huyo Mtaa wa Mazimbu Road Kihonda Mkoani hapa kwa lengo la kumfariji Sambamba na kunusanusa habari kufutia Ustaa wa Marehemu Ngwea.

 

Mwandishi alipofika alikaribishwa vizuri na Bi Mkubwa huyo na baada ya Maongezi Mama huyo alisema.

 

”Shekidele Mwanangu kaondoka najua unapicha zake nyingi za Uhai naomba tafuta moja nzuri nikuzie kisha iweke kwenye Fremu ili niweke hapa  Sebreni”alisema Mama huyo Mcha Mungu, ambaye ni Mwenyekiti wa Moja ya Vigango vya Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Monica Kihonda

 

Mpiga Picha wa Mtandao huu alitii Ombi hilo na siku iliyofuata alimpelekea Picha hiyo, Mara baada ya kuipokea  aliangua Kilio kwa Uchungu huku akimtazama Kamanda wake huyo aliyezima ghafra kama Mshumaa.

’Bwana ametoa na Bwana ametwa Jina lake lihimidiwe.

  Tangulia Kamanda tutaonana badaye.

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...