Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Mara baada ya kukamilika kwa lbada ya maombezi ya kumbukizi ya Mwaka 1 wa kifo cha Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini Albert Mangweha’Ngwea’ iliyofanyika nyumbani kwao Kihonda Mazimbu Road Mwaka 2014.
Siku hiyo hiyo usiku Uongozi wa Ukumbi Maarufu Mkoani Morogoro Samaki Sport Maarufu Samaki Samaki uliopo Kihonda Bima chini ya wakurugenzi wake Mapacha wawili Dada Farida na Mumewe Fujo Kilususu nao waliandaa hafra ya kumbukizi ya Mwaka mmoja wa kifo cha Msanii huyo.
Kwenye Event hiyo iliyoratibiwa kisome ilihudhuriwa na Mastaa kibao kutoka Dar na Moro akiwemo Simba wa Morogoro Mtu pori Seleman Msindi’Afande Sele’ anayeshikilia taji la Ufalme wa Mashairi nchini’Mfalme wa Ryames aliyotwa mwaka 2004 Ukumbi wa Diamond Jijini Dar.
Afande Sele ‘ Mshua Master Baba wa watoto 2 Tunda anayesoma Mwaka wa Pili Chuo Kikiku cha Sokoine’SUA’ na Asante Sanaa anayesoma la 7 Shule ya Msingi Nguzo alipopewa nafasi ya kuimba kama kawaida yake alitunga mashairi makali ya kumzungumzia Ngwea.
.
Mashairi hayo yalimgusa Mama Mzazi wa Ngwea Bi Denisia Mangweha ambaye aliamua kupanda jukwaani na kumtunza Mtu Pori huyo mwenye Chaka lake Kijiji cha Kibwe juu ya Milima ya Uluguru.
Afande Sele anayetumia Jina la Afande hii ni kutokana na Msanii huyo kuwahi kuajiliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania’JWTZ’kabla ya kuondoka na kujiunga na Sanaa,alishindwa kujizuia na kujikuta akimwanga Chozi baada ya kumshuhudia Mama Mangweha naye akimwaga chozi baada ya kuguswa na wimbo wa Afande kama wanavyoonekana Pichana.
No comments:
Post a Comment