Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, May 11, 2022

MICHUANO YA VIJANA YAZIDI KUSHIKA KASI MORO

LENGO LIMETIMIA.

Vipaji vinazidi kuibuliwa kwenye michuano ya Vijana chini ya miaka 20 inayoendelea  uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.

Michuano hiyo inayovuta hisia za mashabiki  imeandaliwa na chama cha soko Wilaya ya Morogoro.













 




Kocha Mkuu wa Kikosi cha Pili cha Maafande wa Ruvu Shooting Rahim Madega kinachoshiri ligi ya Vijana chini ya Miaka 20 ‘Under Twenty 2022’akiwa bize kwenye Bench akitoa maelekezo kwa Vijana wake walipopambana na Vijana wa Black Viba kwenye Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro katika mchezo huo uliokuw amkali kwa muda wote wa dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. 

 

 

MORO YA VIPAJI.

 

Kipa namba moja wa kikosi cha Pili cha Ruvu Shooting Mussa Mlowa akizungumza na Kipa namba moja wa Black Viba mara baada ya gemu ya Viba na Ruvu kutamatika Makipa hao toka utoto wao waliibuliwa vipaji vyao na taasisi ya Moro Kids. Viba inawachexzaji zaidi ya 4 wanaotokea Moro Kids huku Ruvu wakiwa na wachezaji zaidi ya 7 wanaotokea Moro Kids.

 

Kwenye mchezo wa jana kati ya Ruvu na Moro Kids ulitamatika kwa Ruvu kuichapa Moro Kids kwa bao 1-0 huku bao hilo pekee likifungwa na Yahaya Hamis Machupa aliyejiunga na timu hiyo msimu uliopita akitokea Moro Kids na jana ameiadhibu timu iliyoibua Kipaji chake.

 

Kipa Musa Mlowa ni ,Mkazi wa Mji Mpya ambaye ni Mjukuu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mji Mpya ambaye pia alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Marehemu Mwinyimvua Mlowa. Yahaya Machupa ni Mkazi wa Mwembesongo kwa Mzee Machupa.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...