Baadhi ya Wanandishi wa habari pamoja na Wanafunzi wa Vyuo vya uwandishi wa habari wakimsikiliza mgeni rasm
.....Mh Abood aakitoka ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyeji wake Mkilanya
Mh nAbood akipiga Picha na Waandishi wakongwe wa Mkoa wa Morogoro
Mwenyekiti wa Cha =ma Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya kushoto. akizungumza na Mh Abood mara baada ya haffa hiyo kutamatika ukumbi wa Savoy
Katibu Mkuu wa Cha cha Waandishi wa habari Mkao wa Morogoro Lilian Lucus Kasenene Kulia akizungumza na Mh Abood
Mwanfishi Mwandamizi wa Magazeti ya Mwananchi Mkoa wa Morogoro Madam Hamida Shariff akitoa maelekezokwa muhudumu wa chakula
Mtangazaji Mkongwe nchini Bujaga lzengo Kadako'Baba Askofu' akichukua Menyu kwenye hafra hiyo. lfahamike Mzee Kadako aliwahi kutanagza Redio Tanzania kwa sasa TBC LTV na badaye akaja Moro kujiunga na Abood Media kabla ya kutimkia SUA Media pia ya Morogoro ambapo aliduku huko mpaka alipostaafua hivi karibuni
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood ameahadi kuchangia Ujenzi wa Jengo la kisasa la Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ linalojengwa eneo la Kimbwe Juu ya Milima ya Uluguru Jirani na Ofisi ya Wamo Mkoa wa Morogoro.
Mh Abood ambaye pia ni Mfanyabiashara Maarufu nchini Tanzania akimiliki Viwanda, Mabasi, Malori na Vyombo vya habari alitoa ahadi hiyo jana kwenye Maadhimisho ya Vyombo vya habari duniani yanayofanyika kila mwaka Mei 3.
Waandishi wa Morogoro waliradhimika kufanya maadhimisho hayo jana Mei 9 kwenye Ukumbi wa Savoy kufuatia Viongzoi wao wa ngazi za juu kushiriki kwenye madhimisho hayo yaliofanyika Kitaifa Jijini Arusha yalihudhuriwa na Vyama vya waandishi wa habari kutoka nchini zote 54 za Afrika na mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika Mei 3 alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan’Maarufu Mama Samia.’
No comments:
Post a Comment