Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, May 8, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU JUMAPILI YA LEO MEI 8 UNATOKA KWENYE KINYWA CHANGU NA SI KWENYE BIBLIA.



 


 

“Ndoto walizokuwa nazo, ndugu jamaa na Marafiki zetu, zimefifia majira ya saa 6 usiku kabla ya tamanio lao la kuiona siku mpya ya leo May 8 halijatimia, hatunao tena tunajiandaa kwenda kuwapunzisha chini ya ardhi kwenye makazi yao Mapya.

 

Safari yao hapa dunia imefika kikomo wanaelekea kwenye hukumu ya Mungu kupitia matendo yao waliyoyafanya hapa duniani kama wamefanya matendo mema watakaa mkono wa kuume wa Mungu kwa maana ya Pepo ya Milele na Kama wamefanya matendo mabaya wanaketi mkono wa kushoto kwa maana Jehanamu kwenye mateso ya Milele.

 

Kwetu sisi tuliopewa kibari cha kuamka siku ya leo tukiwa na afya njema Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ana makusudi nasi.

 

Tujisahihishe tulipo kosea kwa lengo la kuiandaa kesho yetu kupitia mema yetu na si mabaya yetu ili tamanio letu la kuishi  Pepo ya Milele litimie.

 

 Tulihadaike na tama za hapa duniani tukumbuke kuna maisha mengine tena mazuri zaidi ya haya, sote tumashahdi kuna matajri wangapi waliokuwa wakiishia maisha ya kifalme hapa duniani wamekufa na kuacha utajiri wao hapa hapa duniani wamezikwa na Sanduku kwa Wakristo wa dini nyingine wamezikwa na Vipande 3 vya sanda imekwenda roho yao pekee kwenye hukumu ya Mungu.

 

Kwa leo mtumishi wa Mungu naishia hapa, panapo majiliwa ya Mwenyezi Mungu tukutane Jumapili ijayo kwa mada nyingine ya neno la Mungu.

Nawahusia na kuihusia nafasi yangu kutenda mema na kuacha mabaya."

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...