Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, May 13, 2022

DOGO WA MIAKA 17 AONYESHA KIWANGO CHA HALI YA JUU MCHUANO YA VIJANA ATUNZWA PESA.


Dogo Daud bhana akitoa pasai ya kisigino huku akielekea mbele
Beki kisiki wa Save Talents Hassan Daud mwenye umri wa mika 17 akiruka hewani kuondosha mpira wa hatari ulioelekezwa lengoni mwake, huku akimuacha mshambulia mrefu wa Viba akikosa la kufanya
...Dogo huyo akiambaa na mpira huku mshambuliaji wa Viba akimkaba kwa macho
Kiongozi wa timu ya Save Talent mwenye kofia akiwauzi mashabiki kuongea na mchezaji wake
Mhadini wa MDFA Kaini Patrick akimpa pesa Dogo huyo baada ya kuvutiw ana kiwango cheke


 Shabibi wa timu ya Black Viba aliyefahamika kw ajina la Dogo Menti aliamua kushuka jukwaani na kusogea jirani na uwanja kushuhudia vitu adimu vinavyofanywa na beki wa timu ya Save Talents Hassan Daud


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro,

 

MICHUANO ya Vijana chini ya miaka 20’Under Twenty 2022’iliyoandaliwa na chama cha Soka wilaya ya Morogoro’MDFA’ inazidi kushika kasi kwenye uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.

 

 

Katika michuano hiyo yenye lengo la Kuibua na kuendelea Vipaji vya Soka kwenye wilaya hiyo,malengo hayo yanaendelea kutimia kufuati Vijana wengi kuonyesha Vipaji vya hali ya juu.

 

Miongoni mwa Vijana hao ni Kinda Hassan Daud mwenye Umri ya maiaka 17 anayekipiga timu ya Save Talents ‘Under 20’ yenye Maskani yake Tubuyu Manispaa ya Morogoro.

 

 

Kinda huyo anaye soma Kidato cha 4 Sumaye Sekondari iliyopo Pande za Bingwa jana alikuwa kivutio  kwa mashabiki baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo kati ya timu yake  dhidi ya timu ngumu ya Black Viba.

 

 

Daud anayacheza beki 3 aliwadhibiti wachezaji maarufu wa Viba kama Vile Omary Jira ambapo licha ya umbo lake dogo  alifanikiwa kuwadhibiti washambuliaji  wa Viba inayojianda kushiriki michuano ya  Clouds Media’Ndodo Cup’ iliypangw akuanza kutimua vumbi mei 20 kwenye viwanja vya mitaani jijini Dar.

 

  Licha ya ufupi wake’asmbapo baadhi ya mashabiki walidai hiyo ni mbegu ya kiluguru dogo huyo aliruka hewani kuokoa mipira ya juu akiwapita wachezaji warefu wa Viba kama anavyoonekana Pichani.

 

Pia alionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki na kuucheza mpira atakavyo huku akitoa basi za manjonjo ikiwemo tukio la kutoa basi ya nyuma huku akielekea mbele kama anavyoonekana Pichani.

 

 

Baada ya gemu hiyo kutamatika kwa  Viba kuwatandika Save Talents kwa bao 4-2 baadhi ya mashabiki walishuka jukwaani na kumtunza pesa dogo huyo miangoni mwa watu walivutiwana kiwango cha dogo huyo na kuamua kumtunza pesa ni pamoja na Mhazini Mkuu wa Cha cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’ Kaini Patrick ambaye pia ni Meneja wa timu ya Pam Fc  Pichani akimkabidhi Pesa dogo huyo.

 

Katika hatua nyingine wakati Mwandishi wa Mtandao huu akifanya mahojiano na dogo huyo kundi la watu lilivamia eneo hilo kwa lengo la kutaka kuzungumza na dogo huyo, baada ya kuona hivyo kiongozi wa Save alifika eneo hilo na kuwazuia watu hao kuongea chochote na mchezaji wao kama wanavyoonekana Kipichani  kulia mwenye Kofia’Kapero’.

 

lli kuweka sawa minongono ya mashabiki waliodai kwamba umbo la dogo huyo ni la kabila la Waluguru ambao wengi wao huo ni wafupi alipotakiwa kutaja kabila lake dogo huyo alisema yeye ni Mpogoro wa lfakara.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...