Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 16, 2022

BAADA YA KUKOSEKANA GARI LA WAGONJWA MCHEZAJI AKIMBIZWA HOSPITAL NA BODA BODA.






 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

WAKATI Bodi ya Ligi ya shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’kupitia Kamati yake ya Masaa 72 ikitarajiwa kuketi hivi karibuni  kutoa maamuzi ya mchezo wa Ligi kuu  ulioshindwa kufanyika wiki iliyopita baada ya kukosekana kwa gari la Wangonjwa ’Ambulance’ Uwanjani ya llulu Mkoani Lindi kati ya wenyeji Namungo na Mbeya Kwanza.

 

Juzi Mchezaji wa timu ya Moro Kids’Under Twenty’ Alexander Simon alipoteza fahamu kwa muda baada ya kugongana kichwani na mchezaji wa Chamwino Youth ‘Under Twenty’  Ruben Renatus na kukimbizwa hospital kwa usafiri wa Boda boda baada ya kukosekana kwa gari la wagonjwa uwanja wa Saba Saba kwenye michuano ya Vijana chini ya Miaka 20 yaliyoandaliwa na Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’ waliotii maelekezo ya Uongozi wa Juu wa TFF Taifa ya kuvitaka vyama vyote vya Wilaya ya Mikoa nchini kuandaa michezo ya Vijana na Soka la Wanawake kwenye maeneo yao.

 

Baada ya wachezaji hao kugongana  vichwa  wakigombea Mpira wa juu kwenye mchezo huo uliotamatika kwa Chamwino kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

 

Renatus wa Chamwino alipata huduma ya kwanza na kuendelea na mchezo huku Simon wa Moro Kids licha ya kupatiwa huduma ya kwanza hali yake iliendelea kuwa mbaya hivyo  alikimbizwa hospital kwa usafiri wa boda boda akiwa amepakatwa kama anavyonekana Pichani.

 

Wakati mchezaji huyo anatolewa uwanjani kwa msaada wa mashabiki, wachezaji wa Chamwino na Moro Kids, baadhi ya wachezaji wa Moro Kids waliokuwa wanjani wakishuhudia mwenzao anapanda boda boda waligubikwa na simanzi huku wakionekana kukosa amani kwa muda, hata hivyo badae walikaa sana na kuendelea na mchezo.

 

Ligi hiyo ya Vijana inashirikisha zaidi ya timu 20 kutoka Wilaya ya Morogoro na timu 3 kutoka wilaya na mikoa mingine ziliomba kushiriki ligi hiyo inayovuta hisia za mashabiki Manispaa ya Morogoro kufuatia Vipaji vinavyonyeshwa na Vijana hao.

 

Timu hizo tatu ni pamoja Kilombero Soccer Net kutoka Wilaya ya Kilombero. kikosi cha Pili cha Ruvu Sooting, kutoka Mlandizi Pwani na Pwani Sports Foundation.

 

 Awari kikosi cha Pili cha Mtibwa B ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Vijana wa timu zinazoshiriki ligi kuu waliomba kushiriki ligi hiyo na kuwekwa kwenye ratiba lakini dakika za mwisho walitangaza kutoshiriki michuano hayo.

 

Kanuni za TFF kwenye michezo mbali mbali ikiwemo Ligi Kuu inaelekeza kwamba Msimamizi wa kituo kuzuia mchezo kufanyika iwapo hakutakuwa na gari la wangonjwa uwanjani, kipengere hicho kimelenga kulinda afya za wanamichezo wote waliokuwemo uwanjani hapo wakiwemo Wachezaji, Waamuzi, na Mashabiki.

 

Kanuni hiyo imeendelea kudadavua kwamba mwenyeji wa mchezo husika ndio anayepaswa kuandaa gari  la wangonjwa pamoja wa watoto wanaookota Mipira ‘Ball Kids’ kama huduma hizo hazitakuwepo uwajani mchezo utavunjwa na timu ngeni itapewa ushindi wa Point 3 na mabao 3

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...