Sadi mwenye Mic aki Rap sambamba na wananguaji w aband ya Waluguru Og
Sad sasa kati akionyesha Manjonjo ya Spain kwa Benzema wa Madrid
Sad akiimba wimbo wa Ani aliyowahi kuimba akiwa na Killer Boy band ya Levent Musca
Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.
MTANZANIA Mwana Morogoro anayeishi nchini Hispania Sadi Bongisa ljumaa iliyopita ameuwasha moto na band ya Waluguru Original.
lfahamike Sadi kabla ya kutimkia Spain takribani miaka 10 iliyopita alikuwa akiitumikia band ya Levent Musca ya Mkoani hapa akiwa Sambamba na Deogratius Aruphonsi’Killer Boy.’
Band hiyo ya Levent ilikuwa ikimilikiwa na lnjinia Charles Madinda aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Morogoro ‘TANROADS’
Baada ya Mzee Madinda kufariki dunia Mwaka 2014 band hiyo ilisambaratika, Killer boy alipata zari akaenda Dubai na kigogo Maarufu Mkoani Morogoro Mbena Malumbi wakanunua Seti ya vyombo vya Muziki vya kisasa.
Baada ya kurejea nchini Waluguru hao Malumbi na Killer walianzisha band waliyoipa jina la kabila lao Waluguru Original iliyokuwa ikipiga kwenye baa ya Chilakale iliyopi pande za Bingwa Mkoani hapa baa hiyo ya kisasa ilimilikiwa na Mzee Mbena Malumbi.
Pigo miaka michache mbele Mkoa wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla ikitetema baada ya kupokea taarifa kwamba Mzee Malumbi aliyekuwa akitokea nje ya nchi aliuwawa uwanja wa ndege Dar kwa kupigwa Risasi na watu wasiojulikana.
Baada ya kufariki dunia baa ya Chilakale ilifungwa huku band ya Waluguru Og ikiendelezwa kwa mafanikio makubwa na Jembe Killer Boy.
Sadi Bongisa baada ya kurejea nchini aliamua kutinga Band ya Waluguru na kuimba nyimbo kadhaa alizowahi kuimba na Killer Boy wakiwa Levent Musca.
Akizungumza na Mtandao huu mara baada ya kushuka jukwaani Sadi Bongisa alisema.
” Kwa niaba ya watanzania wanaoishi nchini Hispania nikupongeze sana Shekidele kwa kazi nzuri unayoifanya sisi tunaoishi nje ya nchi tunafuatilia sana Mtandao wako kupata habari za hapa nyumbani.
Wewe ni shahidi nimeondoka hapa nchini Band yetu ya Levent Musca haijafa hivyo ujio wa band ya Waluguru chini ya Killer Boy nimejua kupitia Mtandao wako nikiwa Spain napitia Mlala Nje naona shoo za band mbali mbali za hapa Moro”alisema Sad ambaye baada ya sikuu za Paska na ldd atarejea nchini Hispatan.
Wajanja hawapo Dar Pekee hata Morogoro pia wapo Mbali na Sadi kesho nitataja marafiki zangu zaidi ya 7 walitimkia kihalali Ulaya na Marekani wakitokea hapa Morogoro.
No comments:
Post a Comment