Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, April 15, 2022

NINI DAR HATA MORO PIA KUNA WAJANJA.


           Mandhari nzuri ya Mlima wa Uluguru 'Ever Green'


 
                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 
 
Jana kwenye stori ya Mlala nje niliahadi kuwataja Marafiki zangu Wajanja waliofanya mipango timilifu kutoka hapa Morogoro na kufanikiwa kutimkia Ulaya na Marekani wanakoishi Mpaka sasa.
 
Kwa hapa Morogoro namini wako wengi waliofanya hivyo lakini kwangu mimi nitawataja Marafiki zangu nilioishi nao Maeneo ya Mji Mpya ambao Mpaka sasa licha ya kuishi huko Mbele bado nawasiliana nao Mubashara wengi wao wakiwa wadu wa Mtandao huu. 
 
Wana Morogoro hao hanaosihi huko duniani ni Adam Mlanzi na Eneli Challo Mnyausi, hawa wanaishi Marekani. Bob Tiger na Hassana Banda. 
 
Wako Uingereza, Mashaka Ngedele’ Brazir. Abdallah Ngedele. ltalia, Sadi Bongisa Hispania na Mwanahamisi anayeishi Dubai.
Nimelazimika kufunguka hivi kwa sababu kuna baadhi ya watu wachache wanaoishi jijini Dar wanaamini wajanja wote wako Dar na huku Mikoani hakuna Wajanja. 
 
Hata katika Maisha yetu ya kawaida hilo limejitokeza ‘live’ binafsi nimekumbana na kadhia hiyo. 
 
Kuna Waandishi wenzangu wawili Wanaoishi Dar nimewaingiza kwenye kundi hilo kwa sababu za kiuwanaume sitawataja Majina.
Desemba Mwaka Jana Mwanahabari Mwenzangu ambaye hivi karibuni alikuwa Afisa Habari wa Yanga alinipigia simu akiomba nimsaidi Mwanaye ajiunge na kidato cha kwanza shule ya Sekondari Mzumbe. 
 
Nilifanya hivyo hatimaye alifanikiwa chaajabu baada ya kufanikiwa katumia nguvu kunikwepa, Januari kamreta Mwanaye shule baada ya kutoka Mzumbe na gari lake kapita Msamvu Jua kwa Jua kurejea Dar bila hata kunijuza kwamba Mtoto wetu ameanza shule. 
 
Licha ya kwamba nilishapata taarifa kwamba dogo anaendelea kupiga kitabu School hiyo ya Vipaji Maalumu juzi nilimpigia simu kwa lengo la kumsalimia kwa kejeri kajistukia alivyopokea simu tu kasema.
 
”Du Shekidele niko Kahama wiki hii narejea Dar nikifika hapo Moro nitakupigia.
 
”Nikamjibu kwa kejeri kwamba kwa sasa sipo Morogoro hivyo asihangaike kunitafuta.
 
Jamaa huyo kajiona yeye ni Mjanja wa Dar mimi niliyemsaidia kaniona ni Mjinga wa Morogoro na hisi huo aliofanya ni Utopolo.
Kuna Mwanandishi Mwingine Mtunzi wa Hadithi kwenye Vitabu na Magazeti ya Udaku akiwa Dar alinipigia simu kaniomba ni msaidie Mambo 2 Moja nimuunganishe na Mameneja wa Radio Abood na Planet Radio kwa lengo la kufanya Vipindi vya kutangaza vitabu vyake kwenye Redio hizo Maarufu Mkaoni Morogoro. 
 
Pili nimtafutie hotel nzuri ambayo yeye na wasaidizi wake watalala siku 3 bure, akisema nafaida ya Mwenye hotel atamtangaza kwenye vipindi hivyo Redioni na kwenye Hadithi zake Pendwa. 
 
Himefanikiwa kukamilisha Mambo hayo.nimemunganisha na Mameneja wa Redio hizo kafanikiwa kupewa Vipindi.
Pili nilifanikiwa kuongea na mmiliki wa hotel ya Motel 8-8 iliyopo Maeneo ya Nane nane kapewa vyumba 2 kalala siku tatu bure, Chaajabu kaondoka bila hata kuniaga nampigia simu hapokei.
Kajifanya Mjanja wa Dar mimi ni Mjinga wa Morogoro. 
 
lfahamike kwamba sio wote wa Dar wenye tabia hizo za hovyo, Kuna Waandishi wengi wa Dar waliofika hapa Moro waliomba Msaada wangu niliwasaidia pale nilipoweza nao walirudisha shukrani na tukaagana vizuri kwa lengo la kuendeleza ushirikiano, hata mimi ninapokwenda Dar nikipata mkwamo sehemu huwa nakimbilia kwa Waandishi wenzangu wananisaidia. 
 
Hii ni Ngumu Kumeza Shekidele hana hatia katema nyongo kazi iendelee,
 
"Karibuni Mji Kasoro Kahari,
Morogoro.Hakuna Migogoro, Mtalala kwenye Magodoro"

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...