Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, April 12, 2022

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI. BAND YA WALUGURU OG YATIKISA MAJIJI YA MWANZA, ARUSHA NA DAR.



Mnenguaji nyoya wa Band ya Waluguru Og Sinyorita akikataa Style ya Mchezaji wa Yango Mkongomani Mayele, wakati Picha ya chini akimwambia Mlala nje kwamba anaizimikia Style ya Mchezaji wa Simba Othuman Sakho

Mmiliki wa band ya Waluguru Og Deogratius Aruphonce Maarufu Kileer Boy akifanya yake jauzi ljumaa






 



                    Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

BAADA ya kuuwasha Moto Mkali na kuacha historia katika Majiji ya Mwanza na Arusha, Band ya Waluguru Original wamepata Mwaliko wa kuuwasha Moto katika jiji la Maraha la Dar es salaam.

 

Akizungumza na Mlala Nje juzi ljumaa kwenye Ukumbi uliopo katikatika ya Mji wa Morogoro Kiongozi wa Band hiyo Deogratius Aruphonce Maarufu ‘Killer Boy’alisema.

 

 

”Hivi karibuni tulifanya Shoo katika Majiji ya Mwanza na Arusha Mei 28 tumepata Mwaliko kufanya shoo jijini Dar es salaam ukipata nafasi Shekidele twende wote Dar ukashuhudia Moto tutakao uwasha huko”alisema Killer Boy ambaye ndiye Mmiliki wa Band hiyo.

 

Katika shoo  hiyo ya Ijumaa Mwana Morogoro anayeishi nchini Hispani ambaye aliwahi kuimba Band Moja na Killer Boy Miaka ya 2008 kabla hajatimkia Hispani Wiki hii amerejea nchini na ljumaa alipewa nafsi na Killer Boy akifanya yake jukwaani.

 

Habari kamili na Picha za Mtanzania huyo anayeishi nchini Hispani zitaruka hewani hivi Punde hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...