Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, April 10, 2022

JUMBE WA MUNGU LEO JUMAPILI


 

1 PETRO 2-11

“Wapenzi nawasihi kama Wapitaji na Wasafiri, Ziepukeni tama za Mwili Zipiganazo na roho”Hilo ndilo neno letu la Leo Jumapili ya April 10 kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia.

 

Neno hili la Mungu linatufundisha kwamba tuziepuke tamaa za Mwili zipiganazo na roho zetu.

 

Wapenzi wasomaji wa Mtandao wa Shekidele na wasihi na kuihusia pia nafsi yangu kwamba inafaida gani Starehe ya dakika 5 ikuchonganishe na Mola Wako na kukuharibia kesho yako.?

 

 

Baadhi wamediliki kuvunja ndoa zao kwa tamaa za Mwili na Pesa wakijisahaulisha kwamba hapa duniani tu wasafiri tukisafiri kuelekea Kwa Mungu ambako huko kuna maisha Mengine tena marefu zaidi  ya haya ya hapa duniani.

 

Itakusaidia nini kuvunja ndoa yako au kumsariti Mpenzi wako kwa tamaa za Mwili au Pesa zitakazofanya uishi kifalme hapa duniani huku kesho ukifa pesa hizo unaziacha hapa duniani kwa wakristo Unazikwa na Sanduku hata likiwa la thamani ya miliomi 5 litaliwana mchwa ndani ya Kaburi kinachokwenda kwa Mungu ni roho yako pekee  kwa Waislamu unazikwa na zipande zitatu vya Sanda..

 

Mwenye Masikio na asikie asiye na Masikio[…………]

                    CAPTION

Mwandishi wa habari hizi akisafiri kutoka Morogoro Mjini kuelekea Mikumi kwa usafiri wa Pikipiki akikatiza kwenye Hifadhi ya Wanyama Wakali Kama Simba Chui na Tembo lakini licha ya changamoto hiyo Mungu amemsaidia amevuka salama kwenye hatari hizo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...