Maisha Mapya
“Mimi sio mkali wa kuosha mafuso Tu hata kusakata Sebene najua'
Ndivyo anavyoonekana kusema Muosha Magari Maarufu Mkoani Morogoro Jangara wa Kilosa. anayepiga kazi kando kando ya Mto Morogoro daraja la Shani Sinema akionyesha umahiri wake wa kusakata Sebena akishindano ya wanenguaji wa band Maisha Mapya
Husna Ramadhan akizidi kuuwasha Moto 5 Mnenguaji Mahiri wa band ya Maisha Mpaya Husna Ramadhan ambaye mwaka jana akiwa na Marehem Tatu walijiunga na band ya Maisha Mapya wakitokea FM Academia ya jijini Dar akiwajibika jukwaani wiki end iliyopita.Picha ya chini
Mnenguaji ingizo Jipya wa band ya Maisha Mapya Kavera a.k.a No ya Siri akiuwasha Moto wakati alipotambulishwa kwa mara ya kwanza na band ya Maisha Mpya
Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.
BAADA ya kufiwa na Menguaji wake Mahiri siku za hivi karibuni Marehemu Tatu, bendi Pendwa ya Maisha Mapya wikiend iliyopita imetambulisha wamenguaji wawili kutoka jijini Dar es salaam.
Wanenguaji hao wakali wa kukata ‘nyonga’ ni Mwanadada Hamida a.k.a Mama Segele na Mkaka Kavela a.k.a No ya Siri utambulisho huo umefanyika alhamisi iliyopita ndani ya Ukumbi wa JKT Bwalo la Umwema uliopo jirani na Uwanja wa Jamhuri.
Utambulisho huo ulishuhuidiwa na Mwanamuziki Mkongwe nchini Muumini Mwijuma ‘Kocha wa Dunia’ ambaye pamoja na Mambo mengine amesifu uwezo mkubwa wa wasanii wa band hiyo ya Maisha Mapya.
”Morogoro kuna Vipaji vya kila aina ama kwa hakika band hii ya Maisha Mapya inawanamuziki wenye Vipaji vikubwa sana hasa huyu dogo anayepiga gitaa la Solo amenivutia mno”alisema Mwijuma huku akimshika bega mpiga gitaa huyo anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 20.
No comments:
Post a Comment