Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, April 2, 2022

SADAKA ZA IBAZA ZA MSIBANI ZAZUA KIZAA ZAA,

 Mwandishi wa Mtandao huu Kulia akizungumza na aliyekuwa Askofu Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Telesphor Mkude

 

Mwandishi wa Mtandao huu akizungumza na Askofu wa KKKT Jimbo la Morogoro Job Ole Mameo

                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.  

Mpendwa Msoma wa Mtandao Pendwa wa Shekidele kila Jumapili huwa naweka jumbe wa neno la Mungu.

 

Jumapili ya leo kuna mabadiliko kidogo kuna stori inayohusiana pia na Mambo ya kanisa hivyo twende pamoja kusoma habari hiyo.

Baadhi ya Wananchi mkoani hapa,wameshindwa kujizuia na kuamua kutoa manung’uniko yao  wakilalamikia baadhi ya Viongozi wa dini kuchua Sadaka zote zinazotolea kwenye lbada au Misa Takatifu ya Kumuombea Marehemu.

 

Wiki iliyopita Mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye pilikapilika za kusaka Matukio alishuhudia wananchi  wakilumbano kuhusiana na jambo hilo.

 

Kundi moja lilipinga vikali Mapadri na Wachungaji kukomba Sadaka zote, huku kundi linginge likiunga mkono Viongozi hao kuchukua sadaka hizo.

”Sio sawa lbada ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Mfiwa Padri anakuja kuongoza lbada hiyo watu wanatoa Sadaka kwa ukamilifu baadae Padri anachukua Sadaka zote hampita hata senti tano Mjane wa Marehemu” Alisema Joseph Poul akiwakilisha kundi la wanaopinga.

 

Kwa Upande wake Richard Mdede’Maarufu Makelele akiwakilisha kundi la wanaounga mkono Viongozi wa dini kuchukua sadaka’ alisema  

 

“Kwa uapnde wa kundi langu tunasema ni sahihi Padri kuchukua sadaka zote kwani anakuja hapo msibani kwa usafiri wake hiyo ni kama pesa ya mafuta ya gari pia tufahamu kazi ya Upadri ni taaruma  kama taaruma nyingine”alisme Mdede. 

          MWANDISHI  AINGIA KAZINI.

Baada ya Malumbano hayo Mwandishi wa habari hizi aliingia kazini kwa kuzungumza na Viongozi wa dini hiyo ya Kikristo kwa lengo la kupata ufafanuzi wa Manung’uniko hayo ya Wananchi.

 

Juzi Mwandishi huyo alitinga Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri Tanzania’KKKT’  Usharika wa Mji Mpya ambao ni usharika Mama wa Dayosisi ya Morogoro. Alipotakiwa kuzungumza jambo hilo Katibu Mkuu wa Usharika huo Eliewa Mshana alisema

”Kwa Usharika wetu  Sadaka zote za Msibani tunamkabidhi Mfiwa kama Pole kutoka  kwa waumini wenzie walioshiriki kwenye lbada ya kumuombea Marehemu ifanyika hapa kanisani au nyumbani kwa wafiwa Sadaka zote tunamkabidhi Mfiwa”alisema Mtendaji huyo Mkuu wa Usharika wa Mji Mpya.

 

Baada ya kutoka hapo Mwandishi alipiga gia Pikipiki yake hadi kanisa Kuu la Roman Katoliki Jimbo la Morogoro la Mtakatifu Patrick na kufanikiwa kuzungumza na Paroko wa kanisa hilo Padri Salvinus Kwembe ambapo alipotakiwa kuelezea jambo hilo alisema.

 

“Waumini hao  wanapaswa kujua kwamba kuna Sadaka na Rambi rambi Sadaka ni Mali ya Kanisa na Rambi rambi ni Mali ya Mfiwa. hivyo kwa swali lako Shekidele kwa Utaratimu wa Dhehebu letu la Romani Katolini lbada ifanyika nyumbani kwa Wafiwa au Kanisa sadaka zote ni za kanisa mfiwa hapewi chochote.

          


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...