Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, April 7, 2022

YARIYOJILI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWISHONI MWA WIKI. MWANAMUZIKI ANGULIA KILIO UKUMBINI.

Muumini Mwijua'Kocha wa Dunia' akiendela kumwaga chozi wakati akiimba wimbo wa Kilio cha Yatima
                Mmoja wa mashabiki akimtunza pesa


......Muumini akiendelea kuimba jukwaa moja pamoja na wanamuziki wa Maisha Mapya

 


                                      Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

MWANAMUZIKI mkongwe nchini Muumini Mwijuma’Kocha wa Dunia’ Wiki End iliyopita ameshindwa kujizuia na kujikuta akimwaga Machozi Jukwaani wakati akiimba wimbo wake wa Kilio cha ya tima.

Mwijuma alimwaga machozi hayo kwenye ukumbi wa Bwalo la Umwema unaomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa’JKT’ alipoimba Jukwaa Moja na Band ya Maisha Mapya inayokimbiza kwa sasa Mkoani  hapa.

 

Kufuatia kilio hicho baadhi ya mashabiki wenye machozi ya jirani nao walijikuta wakiangua Vilio huku baadhi yao wakinyongea Jukwaani na kumtunza Pesa ikiwa ni ishara ya kumpa Pole Mwanamuziki huyo.

lkumbukwe Mwijuma aliyewahi kutamba na Band kubwa nchini kama vile  Twanga Pepeta’, Double M Sound. Mchinga Sound na Extra Bongo,kwa sasa  anapiga kazi  Mageze Jazz Band ya Jijini Dar.

 

Aliposhuka Jukwaa Mwandishi wa habari hizi alimfutana Kocha huyo wa dunia na kuumiliza sababu za kuangua Kilio ukumbini ambapo alijibu.” Kaka  Kifo hakizoeleki Mwenyezi Mungu ametuba kusahau lakini tukikumbuka hasa ukiimba wimbo kama huu wa kilio cha yatima uliojaa uhalisia hakika lazima ulio hizo ndizo sababu zilizopelekea mimi kumwaga machozi nikikumbuka vifo vya wazazi wangu”alisema Muumini ambaye ni yatima aliyefiwa na wawazi wake wote wawili.

lnadaiwa Mwanamuziki huyo alitunga wimbo huo  akijibu Manyanyaso aliyofanyiwa na Mmoja wa Mabosi wake wa Moja ya band nilizozitaja hapo juu wakati wa kifo cha Mpendwa baba yake.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...