Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, April 19, 2022

WANANCHI MORO,WANUNG’UNIKA OCD WAO KUHAMISHWA.

OCD Geogna Mtagi akipokea dua kutoka kwa Masheikh
SP Geogna Mtagi aliyekua Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro
...Akizungumza na waislamu waliofurika kwenye shindano hilo

 OCD Georgna[kati] akiwa katika Picha ya pamoja na baadgi ya wanafunzi wa Madrsaa ya Msikiti wa Kingo uliopo Masika Mkoani Morogoro


 

                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

BAADHI ya wananchi Manispaa ya Morogoro wiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii wamechapisha manung;uniko yao kufuatia Mkuu wao wa Polisi Wilaya ya Morogoro’O.C.D S.P Georgna Mtagi kupewa uhamisho.

 

 

Miongoni mwa Wananchi waliotoa maoni yao juu ya uhamishi huo kwa mlengo wa Manung’uniko  kupitia Mtandao wa Facebook ni pamoja na Msanii Maarufu wa Vichekezo na Filamu nchini  Chediel Senzeghe ambaye pia ni Mshereheshaji’MC’Maarufu Mkoani Morogoro.

 

 

Mwandishi wa habari hizi kwa miaka ya hivi karibuni alishuhudia Viongozi wengi wa Jeshi hilo Mkoa wa Morogoro  wakipata uhamisho lakini Wananchi hawakujitokeza hadharani kusema chochote.

 Lakini kwa OCD Georgina  wamejitokeza na kuonyesha masigitiko yao ya Afande wao huyo Kipenzi kuhamishwa kwenye Wilaya yao.

 

 

Kufuatia hali hiyo juzi Mwandishi wa habari hii alimtwangia simu OCD huyo na kuzungumza naye kuhusiana na jambo hilo.

 

”Nikweli limepata uhamisho nakwenda Mkoa wa Manyara, hata mimi nimeona jumbe hizo kwenye mitandao ya Kijamii hii inanitia moyo kwamba nilijitahidi kutenda haki pamoja na kuwa jirana na wananchi”alisema OCD huyo.

 

Alipoulizwa  kuna taarifa kwamba uhamisho huo umekwenda sambamba na yeye kupanda cheo alicheka kisha akakwepa kiaina kujibu swali hilo. Alipoulizwa kama ameshalipoti kwenye kituo chake kipya cha kazi OCD huyo alijibu,

 “Bado niko Morogoro nikiondoka nitakuaga Mwandishi wetu wa habari”

 

 Tetesi ambazo Mtandao huu umezipata zinadai kwamba uhamisho wa OCD huyo unakwenda sambamba na kupandishwa  cheo, tetesi hizo zimeendelea kudadavua kwamba anakwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani’RTO’ Mkoa wa Manyara.

 

Wananchi hao wa Wilaya ya Morogoro wanapaswa kuelewa kwamba kwa watumishi wa Serikali uhamisho ni Jambo la kawaida na lipo kisheria.

 

Ikumbukwe hivi karibuni Mtandao huu  ulirusha habari na Picha za OCD Georgna akiwapa zawadi mbali mbali wanafunzi wa Madrassa ya Msikiti wa Kingo waliofanya vizuri kwenye Mashindano ya kuhifadhi kichwani Quran takatifu.

 

 OCD huyo ambaye kiimani ni Mkristo alikubari Mwaliko wa kuwa Mgeni rasmi kwenye shindano hilo  hakutuma mwakilishi alitinga mwenyewe kwenye Msikiti huo huku Mtandao huu ukimshuhudia akiwasili Msikitini hapo na Usafiri wa Difenda lililojaa Juisi alizogawa kwa watoto wote walioshiriki shindano hilo.

 

Vitabu vya dini vinatueleza kwamba sauti ya Wengi ni sauti ya Mungu mfano watu 9 wakikuzungumzia vizuri kwa mema yako  Mungu anaungana nao anawakuwa  wa 10.

Huku  watu 9 wakikuzungumzaia Vibaya’ Kwa maovu unayoyafanya Mungu pia anajumuika nao anakuwa anakamata no 10 na Malipo yake ni hapa hapa dunia.

 

Hivyo kwa  maneno hayo ya Vitabu vya dini huenda kwa OCD huyo kuzungumzwa vizuri na watu wengi Mungu amekuwa mtu wa 10 na malipo yake ni hayo ya kumpa baraka hapa hapa duniani ya kupandishwa vyeo akiwa angali bado Kijana.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...