Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, April 17, 2022

PADRI ANAYEMILIKI SHULE YA SEKONDARI INAYOSOMESHA YATIMA BURE.


 

 

                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

LEO ni Jumapili ya Pasaka tukisheherekea Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetoa sadaka uhai wake ili  Mimi na wewe unayeamini tuokolewe.

 

 Kawaida ya Mtandao huu kila Jumapili huweka kando habari zote za kidunia na badala yake hutumia siku hiyo kuandika  Neno la Bwana ambalo hulichambua kwa Ufupi kwa lengo la kukumbushana ama kuandika habari inayohusiana neno la Mungu.

 

Hivyo Jumapili ya leo ambayo ni Jumapili ya Pasaka nitamzungumzia Padri Ricardo Henrico Maria Mwenye Asili ya ltaly Raia wa Tanzania ambaye ni Mmoja wa Waanzilishi wa Kituo cha  Radio Ukweli kinachomilikiwa na Kanisa  Kathoriki Jimbo la Morogoro.

 

Chini ya Usimamizi wake Kituo hicho  kilichopo ndani ya  Jengo la Kanisa Kuu la Mt Patrick lililopo jirani na Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

 

Kituo hicho kinaendelea kutoa ushindani Mkali kwa vituo vingine vya Radio Mkoani Morogoro.

 

lkumbukwe Manispaa ya Morogoro  inavituo vya Radio zaidi ya 7 ambavyo ni  Radio Abood. Planet Fm, lmmani Fm, SUA Fm, Top Radio. Okoa Fm, MVIWATA Fm na Radio Ukweli.

 

 Wilaya nyingine za mkoa wa Morogoro pia kuna Vituo vya Radio hivyo licha ya wingi wa Radio hizo Mkoani Morogoro Radio Ukweli chini ya Usimamizi wa Padri huyo kimeendelea kutoa ushindani Mkali huku ikisogeza lnjiri ya bwana kwenye majumba ya watu kupitia masafa ya 92.7 Ukweli Fm.

 

Kila siku za Jumamosi kuanza saa 3 na nusu Mpaka saa 4 asubuhi Padri Ricardo  anayezungumza kiswahiri Fasaha anafundisha neno la Mungu, Jana jumamosi nikiwa nyumbani nilisikiliza kipindi chake ama kwa hakika  nilibarikiwa sana na mahubiri yake.

 

Padri huyo ambaye kutokana na lmani yake ya kidini havai Viatu, nami toka nimfahamu zaidi ya miaka 10 sijawahi kumuona kavaa Viatu  au kavaa suluali na shati mara zote nilimshuhudia na vazi la kanzu.

Pia sijawahu kumuona anatembelea gari kila siku  nilimshuhudia akitembelea  usafiri wa Baiskeri.

 

Baada ya kufanikiwa kueneza neno la Mungu kwa njia ya Radio Padri Ricardo alihamia upande wa Pili wa Elimu, kaanzisha shule kubwa ya Sekondari inayojulikana kwa jina la Alfagem ‘Maarufu shule ya Pekupeku’ kufuatia mmiliki wa shule hiyo kutembea peku peku.

 

Lengo kuu ya Shule hiyo ni kuwafundisha tena wanafundi waliofanya vibaya kwenye Mitihani ya taifa ya kidato cha Pili cha 4 na cha 5 ili waweze kufaulu na kuendelea na masomo.

Kumbe jambo hilo la wanafunzi kuferi na kushindwa kuendelea na masomo lilimumiza sana Padri huyo maumivu hayo yakampawazo lililomsukuma kuanzisha shule hiyo.

 

 ALFAGEMU ndio shule pekee ya kwanza mkoani Morogoro kuludisha matumaini yaliyopotea kwa Madent  walioshindwa kuendelea na Elimu baada ya kuferi Kidato cha Pili,  cha Nne na Kidato cha Sita.

 

Wengi walioludia masomo kwenye shule hiyo yenye walimu wazuri walifaulu na kwenda Vyuo Vikuu.

 

 

Kwa wakazi wa Mkoa wa Morogoro watakubaliana nami kwamba  kila ukifungua Radio za mkoani Morogoro unakutana na matangazo ya shule za sekondari za ‘Open School’.

Wakipiga ‘debe’wanafunzi kujiunga na shule zao lakini hata siku moja hatujasikia tangazo la shule  ya Ricardo ambayo watafiti wa mambo wanadai ndio shule inayoongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi kuliko shule nyingine.

 

 Kufuatia hali hiyo siku za nyuma nilimtafuta Padri huyo kwa lengo la kuzungumza naye.

 

Mungu ni mwema  ghafla nimemuona anakatiza maeneo yangu ya  Mji Mpya akiwa na baiskeli yake akitoka kwenye Kipindi Radio Ukweli akielekea  kweye shule yake iliyopo maeneo ya Nane nane  Mtaa wa Mji Mwema.

Aliponipa nafsi ya kunisikiliza nilizungumza naye hivi.

Mwandishi. Father  tumsifu yesu Kristo. 

Padri Ricardo. Milele Amina.

 

Mwandishi. Najua uko bize hivyo nisikupotezee muda wako kwanza ubarikiwe sana kwa kazi nzuri ya utumishi kupitia.

Radio Ukweli na kwenye shule yako, swali langu ni moja tu ni kweli umetoa ruhusa wanafunzi yatima kusoma bure kwenye shule yango?

Padri. Ni kweli mwanafunzi kwenye udhibitisho wa kufiwa na wawazi wake wote wawili anasoma bure nini niko kwenye huduma ya kusaidia watu na sipo kwa ajiri ya biashara ya kupata faida ya kujinufaisha,hao wanafunzi ninaowalipisha ada pesa hizo zinanisaidia kulipa mishahara walimu. Kuongeza majengo na kununua Vitabu vyao wakujisomeana N.k

Mwandishi Ok Padri R mungu akubariki sana.

Padri. Ubarikiwe na wewe pia.

 

Alisema Padri huyo na kupigia gia baiskeri yake huku akimpungia Mkono Mwandishi wa Mtandao huu kama anavyoonekana pichani.

Picha hii ilisambaa sana kwenye Mitandao ya Kijamii

 

 

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...