Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, April 16, 2022

USIYOYAJUA KUHUSU SHABIKI NO 1 WA SOKA TANZANIA.


 


                                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kwa sasa hapa nchini kuna Mashabiki wengi wa Soka wakiwemo wa timu kubwa za Simba, Yanga na Azam lakini  hakuna shabiki yoyote wa timu hizo aliyeweza kumpiku shabiki wa timu ya Reli ya Morogoro ‘Kiboko ya Vigogo’ Marehemu Hamza Lyamungu aliyefariki dunia takribani Miaka 15 iliyopita.

 

Marehemu Lyamungu na Mwandishi wa habari hizi walikuwa Wanachama Pekee wa Reli  waliopitishwa na Uongozi wa timu hiyo iliyokuwa ikishiriki ligi kuu kusafiri na timu hiyo mikoa mbali mbali ya Tanzania.

 

Lyamungu mbali ya kujichona mwili mzima na kuandika Maneno ya kejeri kwa timu pinzani pia alikuwa kwenye kamati ya Ufundi huku Mwandishi wa Mtandao huu akiwa Mpiga Picha Mkuu wa timu hiyo.

 

Moja ya maandishi ya kejeri ninayoyakumbuka kwa timu mbinza ni Siku  Reli ilipocheza na Milambo ya Tabora tukiwa Uwanja wa Ally Hassan Mwingi Lyamungu alijichora mwilini ‘Mirambo Kumfunga Reli ni sawa na Jaruo kuimba Taarabu’ gemu hiyo ilitamatika kwa Milambo kupokea kichapo cha bao 1-0.

 

 

Kiuharisia Lyamungu alikuwa Shabiki wa Pan Afrika ya Dar na siku Reli ilipocheza na Pani uwanja wa Jamhuri Morogoro siku Moja kabla ya Mchezo  tukiwa mitaani Mashabiki wengi walimuliza Lyamungu atashangilia timu gani kati ya timu yake ya Moyoni Pani na timu yake ya kazi Reli?.

 

 Lyamungu aliwajibu ‘Njooni kesho uwanjani mtaona timu nitakayoishangilia”, Siku ya Mchezo huo Lyamungu alijichora maneno yaliyosomeka ”Mke na Kazi Bora nini?’’huku akiwa bize Uwanjani na timu ya Reli huku akiipa kisogo timu ya Pan.

 

Reli ilipokipiga na Yanga Uwanja wa Taifa kwa sasa  Uhuru uliopo Temeke jijini Dar Lyamungu alisema.

 

“Rafiki yangu nimechungulia nimeona gemu hii ngumu tunaweza kufungwa hivyo katika hali ya kuzunga ngoja leo nijichole maneno ya kukupaisha wewe”.

 

Gemu hiyo ilitamatika kwa timu hizo kutoka sale ya bao 1-1 huku bao la Reli likifungwa na mshambuliaji hatari David Mihambo akipokea Assit ya Mbuyi Yondani.

    USIYOYAJUA KUHUSU LYAMUNGU. Lyamungu ni Mpogolo wa lfakara  Mkristo aliyekuwa akijulikana kwa jina la Godfrey Lyamungu  aliishi na mkewe aliyekuwa muumini ya dini ya Kiislamu kwa miaka Mingi kila mtu aliabudu dini yake.

Badaye Lyambu aliamua kuingia Msikitini na kusilimu baada ya kuchomewa ubani akapewa jina la Hamza na siku chache baadae  wawili hao ‘walipasha Moto kiporo’walifunga ndoa kwa dini ya kiislamu.

 

Nakumbua baada ya Lyamungu kusilimu tajiri Aziz Abood alidhamini maandalizi ya sherehe ya harusi ambapo tulipiga goti tukaufivya mpunga mweupe na mwekundu.

 

La pili usilolijua hukusu Lyamungu katika Maisha yake hajawahi kunywa Pombe aina yoyote licha ya vituko vyake uwanjani.

“Umetangulia Kamanda tutaonana baadae, mimi na wanao Hawa na Said tutakukumbuka daima”  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...