Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, March 8, 2022

SIKU YA MWANAMKE DUNIA,MKUU WA POLISI MORO AGAWA ZAWADI KWA WATOTO WA MADRASSA.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya MorogoroOCD' SP Georgna Mtagi akipokea Dua kwenye hafra ya Maonyesha ya kusoma Quran ya watoto wa Madrassa ya Al Hasaniyyah Msikiti wa Kingo Mkoani Morogoro. 

OCD huyo ambaye kiimani ni Mkristo alikuwa mgeni rasmi kwenye hafra hiyo iliyofana

OCD SP Georgna akiwapa zawadi wanafunzi hao wa Madrassa ya AlHasaniyyah ya Msikiti wa Kingo Mkoani Morogoro






 Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Nibuka Mzeru Kulia akimpongeza OCD Georgna kwa hotoba yake nzuri


                                      Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

LEO March 8 ni Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani, kwa Upande wa Wilaya yetu ya Morogoro tunajivumia kuwa na Mkuu wa Polisi Mwanamke ‘O.C.D’ SP Georgna Matangi.

 

OCD Georgna hana ubaguzi wa Rangi, Jinsia wala Dini, hii imedhihirika juzi Jumamosi licha ya kuwa ni Muumini wa Dini ya Kikristo lakini alikubari Mwaliko aliopewa na Uongozi wa Msikiti wa Kingo kuwa Mgeni rasm kwenye Maonyesho ya watoto  wa Madrassa ya Al- Hasaniyyah ya kusoma Quran kwa kichwa. 

 

Katika hafra hiyo iliyohudhuriwa pia na Mbunge Mstaafu wa jimbo la Morogoro Mh Nibuka Mzeru OCD alivutiwa na Vipaji vilivyoonyeshwa na watoto hao na kuamua kuwapa zawadfi ya Pesa. Akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi OCD Georgna alisema

 

” Ukiwa na taifa lenye watu wengi waliolelewa katika Misingi ya dini uharifu unapungua kama sio kuondoka kabisa kwenye Jamii zetu  kwani watakuwa na hofu ya Mungu.

Hivyo watoto wetu tukiwalea kwenye misingi kama hii ya dini tunajenga taifa la watu Waadirifu”alisema OCD huyo na kuongeza

‘Nimevutiwa sana na Vipaji vilivyoonyeshwa na Vijana hawa kwa kusema maneno ya Mungu kwa lugha ya Kiarabu bila kubabaika, katika  hali ya kuwatia Moyo nimeamua kuwapa zawadi ya Pesa na Juice”alimalizia kusema Mkuu huyo wa Polisi wa Wilaya ya Morogoro ambaye kwenye hafra hiyo alitinga na Difenda huku akiwa ametinga Vazi takativu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...