Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, March 9, 2022

MTOTO WA KIGOGO WA KAMPUNI YA MABASI YA ABOOD ASHUSHA HADITHI NZITO YA MTUME MOHAMAD,

Ustadhi wa kesho Amour Said Boss akisoma Moja ya Haidth za Mtume Muhamad
                 ......Akitunzna Pesa na Mama yake Mdogo

                ,,,Akipewa zawadi ya Pesa na baba  yake Mzazi


                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 
 
DOGO Amour Said Boos Mwishoni Mwa Wiki amekong’anyoyo za waumini wa Msikiti wa Kingo baada ya kusoma kwa ufasaha moja ya hadithi za Mtume Mohamad kwa lunga ya Kiarabu. 
 
Amour anayesoma Madrassa ya Al-Hasaniyyah ya Msikiti wa Kingo mkoani hapa, alifanya hivyo Jumamosi iliyopita kwenye Maonyesho ya kusoma Quran kwa wanafunzi wa Madrassa hiyo yaliyofanya kwenye Viwanja vya Msikiti huo. 
 
Mara baada ya kusoma hadith hiyo dogo huyo alitunzwa pesa na Mama yake Mdogo kama anavyoonekana Pichani, Kama hiyo haitoshi baba mzazi wa dogo huyo Said Boss ambaye ni Kigogo wa Kampuni Pendwa ya Mabasi ya Abood pia alimtunza Pesa Kijana wake kama anavyonekana Pichani akimkabidhi Pesa.
 
Mama mzazi wa dogo huyo Bi Fetrish Adam’a.k.a ,’Mrs Boss’ ambaye naye ni Super Staa wa Mujini hakuwepo kwenye hafra hiyo, huku taarifa zikidai kwamba alipata udhuru na kusafiri nje ya Mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...